Ouattara ashinda uchaguzi huku wakiuonya upinzani

 

Chama tawala cha rais wa Ivory Coast Alassane Ouattara hapo jana kimewaonya viongozi wa upinzani dhidi ya majaribio ya kutoa mwito wa kukabidhi madaraka baada ya kususia uchaguzi uliofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita.

Chama tawala cha rais wa Ivory Coast Alassane Ouattara hapo jana kimewaonya viongozi wa upinzani dhidi ya majaribio ya kuitisha makabidhiano ya madaraka baada ya kususia uchaguzi uliofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita, wakigomea hatua ya rais huyo kuwania awamu ya tatu.

Tume ya uchaguzi ya taifa hilo la Magharibi mwa Afrika lilichapisha matokeo ya awali kufuatia uchaguzi uliofanyika Jumamosi iliyopita yaliyoonyesha Ouattara akiongoza na ambayo hata hivyo yalitarajiwa hasa kwa kuwa upinzani ulisusia uchaguzi.

Makabiliano yalizuka nchini Ivory Coast mwezi Agosti wakati Ouattara aliposema mageuzi ya kikatibaRais Ouattara wa Ivory kuwania tena Urais Oktoba yalimruhusu kuwania awamu ya tatu hatua iliyoibua ghadhabu kutoka upande wa upinzani ambao walitoa mwito wa mapinduzi ya uchaguzi.

Machafuko ya kabla ya uchaguzi yalisababisha vifo vya watu 30 na maandamano ya upinzani yalichochea wasiwasi wa kurejea kwa mzozo wa mwaka 2010 hadi 2011 uliosababisha vifo vya watu 3,000 baada ya rais Laurent Gbagbo kuyakataa matokeo yaliyompa ushindi Ouattara

Mkurugenzi wa chama tawala cha RHDP Adama Bictogo aliuambia mkuano wa waandishi wa habari kwamba chama hicho kinamuonya Affi N'Guessan na washirika wake dhidi ya majaribio yanayoweza kusababisha hali ya kukosekana kwa ustahimilivu. Bictogo alikuwa akimjibu kiongozi wa upinzani N'Guessan, ambaye hapo awali alisema upinzani unayapinga matokeo hayo ya uchaguzi.

Comments