Mwasisi
wa mtandao wa Jamii Forums nchini Tanzania, Maxence Melo amekutwa na hatia
katika shtaka la kuzuia uchunguzi wa polisi hata hivyo ameachiwa kwa sharti la
kutokutenda kosa kama hilo kwa kipindi cha mwaka mmoja.
Bwana Melo pamoja na mwanzilishi mwenza wa mtandao wa Jamii
Forums BwMike Mushi walifuguliwa kesi yenye mashtaka mawili mwaka 2016 katika
Mahakama ya Kisutu. Kosa la kwanza likiwa ni kuendesha mtandao ambao
haujasajiliwa kwa kikoa (domain) cha Tanzania (.tz) na shitaka la pili la
kuzuia uchunguzi wa polisi kwa kutokutoa taarifa za waachama wawili wa mtandao
huo waliodaiwa kuandika madai ya uhalifu kuhusu benki ya CRDB na Mamlaka ya
Bandari nchini Tanzania.
Kwa mujibu wa wakili wa wawili hao Bw Benedict Ishabakaki, Melo
amekutwa na hatia ya shtaka la pili la kuzuia uchunguzi, huku Mike Mushi
akikutwa hana hatia katika mashtaka yote mawili.
Comments
Post a Comment