Na Baraka lusajo- Kalambo
Imeelezwa
kuwa kufuata misingi ya sheria, taratibu na kanuni zinazo tawala suala zima la
uchaguzi wa viongozi ni nyenzo na nguzo muhimu ya amani, utulivu na ukuaji wa
uchumi kwa ajili ya maendeleo ya wananchi na taifa lao.
Wakieleza
kwa nyakati tofauti, watendaji wa uchaguzi ngazi ya vituo na jimbo waliojitokeza
kwa wingi kwenye zoezi la usaili lililofanyika kwenye shule ya wasichana ya Matai
Wilayani Kalambo mkoani Rukwa, wamesema wamefurahishwa na utaratibu huo mpya
kwani unalenga kupata wasimamizi wenye weledi ili zoezi la uchaguzi mkuu wa
Rais, wabunge na madiwani linalo tarajiwa kufanyika tarehe 28 oktoba 2020
lifanyike kwa mafanikio makubwa huku uhuru na haki vikitamalaki nchini kote na
kuivusha nchi ikiwa salama.
Cosmasi
Mbawala ambae ni afisa uchaguzi msaidizi
jimbo la Kalambo , amesema zaidi ya watu
(1700) wamejitokeza katika zoezi la usaili ambalo limefanyika katika maeneo
tofauti ya wilaya hiyo na kusema
mahitaji ni 1376 .
Hivi
karibuni, Kamishina wa uchaguzi taifa balozi Omar Ramadhani Mapuri akiwa kwenye
kikao na wadau wa uchaguzi mkoani Rukwa alisisitiza umuhimu wa vyama vya siasa
na wagombea kuzingatia maadili katika kampeni zao na kuwa taka wananchi
kujitokeza kwa wingi kupiga kura tarehe 28 oktoba kwani maandalizi yote
yamekamilika.
“wakati
tume inaendelea kuratibu, kusimamia na kuendesha uchaguzi huu kwa kutumia sheria
za uchaguzi, vyama vya sisa wagombea na wananchi wanakumbushwa kuwa katika
kipindi hiki, sheria nyingine za nchi hazijasimama hivyo wajihadhari na vitendo
vya matamshi ambayo yanaweza kusababisha vurugu kwa kisingizio cha uchaguzi. Alisema
balozi Mapuli.
Comments
Post a Comment