Na mwandishi wetu kalambodc.
WATOTO wameomba kuwepo na Mabweni katika shule za Sekondari ili
kuondoa uwezekano wa Watoto hao kwenda kupanga vyumba mjini wawapo shuleni ili
kuweza kuondokana na mimba za utotoni.
Ombi hilo limetolewa jana na Wanafunzi wa shule za Sekondari za Mashete,Mtenga,Milundikwa,Mkwamba,Isale,Mkangale,Nkomolo na Nkasi sekondari kwenye maadhimisho ya siku ya mtoto wa kike ambapo wamedai kuwa kitendo cha wao kupanga vyumba mjini ni kichocheo kikubwa cha wao kupata vishawishi vinavyopelekea kupata mimba na kukatishwa masomo yao.
Wakizungumza kwenye mdahalo Maalumu ulioandaliwa na shirika lisilokuwa
la kiserikali la Plan International juu ya Matumizi ya mitandao ya
kijamii kama ikitumika vibaya inaweza kuwapa madhara ya kupata mimba na ndoa za
utotoni bila yao kutegemea walidai kuwa ni kweli lakini kubwa
linalowasumbua wao kama Watoto wa kike ni kukaa mitaani badala bwenini ambako
kuna uangalizi mkubwa.
Akizungumza kwenye mdahalo huo Adolphina Kapembwa
Mwanafunzi wa shule ya sekondari Mkangale alidai kuwa licha ya mitandao ya
kijamii kuwa na changamoto kwao,lakini kubwa ni la kukosekana kwa Mabweni ya
kutosha mashuleni inayopelekea wengi wao kwenda kupannga vyumba mitaani ambako
ukutana na vishawishi vingi ambavyo ukwamisha ndoto zao walizojiwekea katika
maisha yao.
Hivyo aliwaomba Wazazi wao,serikali na Wadau wengine kuliona
jambo hilo kuwa ni la msingi kwa kuhakikisha kuwa katika shule zote za
Sekondari yanajengwa Mabweni ya kutosha kuwawezesha Watoto wote hasa
wa kike wanaishi kwenye Mabweni kuliko na uangalizi mkubwa ukilinganisha na
mitaani kwenye vishawishi vingi.
Benezeth Mtuka kwa upande wake alisema kuwa Mitandao ya kijamii
ni muhimu kwa maendeleo lakini pale inapotumika vibaya ina madhara makubwa hasa
kwa Watoto wa kike bali kinachotakiwa ni Wao wenyewe Watoto kujitambua kuwa wao
ni nani? Na lengo lao nini wawapo shule na kuwa hilo likiwezekana mimba na ndoa
za utotoni zitatoweka kabisa kwa Watoto walio mashuleni.
Mwakilishi wa dawati la jinsia na Watoto Atupele
Hance alisema kuwa changamoto kubwa wanayoipata jeshi la
Polisi ni kupata ushahidi dhidi ya vitendo hivyo na kuwa kama Watoto wenyewe
wangekua Wawazi vitendo hivyo vya mimba za Utotoni ingekua ni ndoto.
Alisema kuwa kama Wasichana wangekua wanatoa taarifa pale
wanapotongozwa ingeasaidia sana kuwawekea ulinzi lakini kitendo cha kukaa kimya
kinawapa nguvu Wanaume cha kuendelea kuwarubuni na mwisho wa siku wanaingia
mitegoni.
Meneja miradi wa Plan International Williamu Mtukananje
alisema kuwa shirika lake kwa kushirikiana na serikali wamekua katika vita hiyo
kubwa ya kukabiliana na mimba za Utotoni na kuwa hivi sasa vita hiyo imeeleweka
kwa jamii bali kinachotakiwa sasa ni ushirikiano toka kwa wazazi kwa maana
ndiyo wamekua wakiharibu kesi hizo pindi ziendapo mahakamani
mwisho
Comments
Post a Comment