Serikali Yatoa Bilion 2.4 Kwa Ajili Ya Ujenzi Wa Miradi Ya Maji’’kalambo.


Na  Baraka Lusajo- Kalambo 

Serikali kupitia wizara ya maji nchini imetoa fedha kiasi cha shilingi Bilioni 2.4 kwa ajili ya ujenzi wa miradi ya maji itakayohudumia zaidi ya wananchi elfu ishirini (20000) katika vijiji 10 vya kata za matai na kilesha huku kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya hiyo ikiwaagiza viongozi  wa serikali za vijiji kuwachukulia hatua kali za kisheria watu wanao lima kwenye vyanzo vya maji.


Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya hiyo Calorus Misungwi, alisema kukamilika kwa miradi hiyo kutasaidia wananchi kupata maji safi na salama kwa wakati wote na kuwataka wananchi kulinda  vyanzo hivyo kwa  kuacha kulima kwenye vyanzo vya maji.


‘’Baada ya miradi hii kukamilika wananchi watapata maji safi na salama kwa wakati wote kwa siku jirani na makazi yao.Aidha hakutakuwa na magonjwa yatokanayo na ukosefu wa maji safi na salama ,hivyo ni muhimu kila mmoja kulinda vyanzo vya maji na kuacha  kulima ndani ya mita sitini.’’Alisema Misungwi.


Mkuu wa Takukuru wilayani humo Lupakisyo Mwakyolile, alisema wamekuwa wakifuatilia miradi hiyo kwa lengo la kuhakikisha   inakamilika kwa ubora unaotakiwa na kwa wakati ili kuwawezesha wananchi kupata  huduma ya maji safi na salama.


Meneja wa RUWASA wilayani humo Patrick Ndimbo, alisema uwepo wa miradi hiyo utawasadia wananchi kuondokana na adha ya kukatika kwa maji.

Alisema kiasi cha fedha shilingi za kitanzania million 402 zimetolewa kwa ajili ya ujenzi wa miradi ya maji katika eneo la singiwe, milion 502,756,819 katika mradi  wa matai na billion 1,441,124,465 katika mradi wa kilesha.

 

 

Comments