Barozi Wa Nyumba Kumi Akutwa Akiwa Ameuwawa.



 Na mwandishi wetu Kalambodc.

Mkazi mmoja wa mtaa wa Nyanya kata ya Msua manispaa ya sumbawanga mkoani Rukwa Teddy Charles  mwenye umri wa miaka 63 ambae ni Barozi wa Nyumba kumi amekutwa  akiwa ameuwawa na mtu au watu wasiofahamika kisha mwili wake kukutwa nje  ya makazi yake.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Rukwa Kamishina Msaidizi wa Polisi Justine Majura Masejo, amsema tukio hilo lilitokea tarehe 25/09/2020 majira kati ya saa 8:00hrs huko Mtaa wa Nyanya Kata ya Msua Tarafa ya Lwiche Manispaa ya Sumbawanga Mkoa wa Rukwa.

‘’Marehemu alikuwa ni mkulima pia balozi wa nyumba kumi, mkazi wa kisiwani amekutwa ameuawa na mtu/watu wasiofahamika. Mwili wa marehemu umekutwa ukiwa nje ya nyumba yake umbali wa Mita 5. Uchunguzi wa awali unaonyesha kuwa marehemu alikuwa na migogoro ya kifamilia. Mtu mmoja ameshikiliwa na Jeshi la Polisi kwa mahojiano kuhusiana na tukio hilo.’’alisema Kamanda Masejo.

Aidha Kamanda wa Polisi Mkoa wa Rukwa Kamishna Msaidizi wa Polisi JUSTINE MAJURA MASEJO anatoa wito kwa wananchi kuwa migogoro yote iwe inatatuliwa kisheria

Comments