Akutwa Akiwa Amefariki Dunia Kwenye Mitalo Ya Maji.’’Kalambo’’

Wananchi katika Kata za Lyowa na Matai wilayani Kalambo mkoani Rukwa wamelaani vikali kitendo cha mwamke mmoja ambae hakufahamika jina wala makazi yake kuuwawa kisha mwili wake kutupwa kwenye mitalo ya maji ya mto Chimilango katika mtaa wa Keleni.

Wakazi maeneo hayo  wamesema  mwili huo  ulikutwa kwenye mtalo wa maji yanayotumika kumwagilia Bustani  za mboga mboga katika mtaa wa Keleni wilayani humo, wamesema waliugundua mwili huo wakati wakisafisha mitalo hiyo.

Mwenyekiti wa mtaa huo Linus Mawela, amesema mwili huo uligundulika wakati watu wakisafisha vichaka kwenye mitalo hiyo na kusema baada ya kuona mifupa waliamua kutoa taarifa kwenye uongozi wa kijiji ambao ulitoa taarifa polisi.

Amesema jeshi la polisi lilifika eneo la tukio na kuwaruhusu wananchi kufanya   madhishi pembezoni na mitalo hiyo, kwani mwili huo ulikuwa haujagundulika kutokana na kuharibika vibaya.

Mtendaji wa kijiji hicho Muhamed Rajabu, amesema mwili huo haujafahamika na   kusema mwili huo ulikutwa katika maeneo ya bustani ambako kuna mitalo ya kupitisha maji kwa ajili ya umwagiliaji.

Mganga mfawidhi wa kituo cha afya Matai Dr.Edwini Mlingi ,amesema katika  uchunguzi waharaka ilibainika kuwa marehemu alikuwa ni wa kike na mwili wake unakadiliwa kuwa  kwenye maji kwa  zaidi ya miezi mitatu.

Comments