Na Israel Mwaisaka,Nkasi
MKUU wa mkoa Rukwa Joakhimu
Wangambo amesema kuwa ataipeleka TAKUKURU kuchunguza matumizi ya fedha Tshs,Mil.300
zilizotumika kujengea hospitali ya wilaya Nkasi.
Akizungumza jana baada ya ukaguzi
wa ujenzi wa hospitali ya wilaya mkuu huyo wa mkoa alidai kuwa haoni sababu ya
hospitali hiyo kuchelewa kukamilika wakati fedha zimetolewa na serikali
ukilinganisha na kasi iliyokuwepo awali.
Hilo lilikuja baada ya mkuu wa
wilaya Nkasi Said Mtanda kumweleza mkuu wa mkoa kuwa hajalidhishwa na
namna ambavyo halmashauri wamezisimamia fedha kiasi cha Tshs,Mil.300 katika
kukamilisha ujenzi kwenye hospitali hiyo na haijakamilika na kuuomba mkoa
kuingilia hari hiyo.
Mkuu wa mkoa kwa upande wake
aliamua kuwakabidhi TAKUKURU kufanya uchunguzi wa jambo hilo na kuwa
matokeo ya uchunguzi huo yatafanyiwa kazi.
Kufuatia hari hiyo mkuu wa mkoa
Wangabo alitoa siku 14 kwa mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya Nkasi
Missana Kwangula kurekebisha kasoro hizo zilizojitokeza na kuwa baada ya muda
huo atarudi kuona maagizo hayo yametekelezwa kwa kiasi gani.
Sambamba na hilo mkuu huyo wa mkoa
amemtaka mkandarasi wa ujenzi wa Tanki la maji mjini Namanyere kuhakikisha kuwa
ujenzi wake unakamilika kwa muda uliopangwa.
Alisema kuwa anasikitishwa na kasi
ndogo ya ujenzi wa tanki hilo na kuwa kwa mujibu wa mkataba ilibidi ujenzi wa
Tanki hilo uwe umekamilika na jamii kuendelea kupata huduma ya maji
Kaimu meneja wa SUASA Emmanuel
Mashauri alisema kuwa ujenzi wa tanki hilo mpaka sasa umefikia asilimia 92 na
kuwa siku chache zijazo kazi hiyo itakua imekamilika na litaanza kutoa huduma
ya maji kwa jamii
Alisema kuwa hadi sasa hari ya
upatikanaji wa maji katika mji wa Namanyere ni asilimia 16 tu na kuwa mradi huo
utaongeza wigo mpana wa upatikanaji wa maji.
Mwisho
Comments
Post a Comment