katika picha ni baadhi ya wananchi wakiwa eneo la madhishi |
Wananchi wa kijiji cha Mbuluma wilayani Kalambo mkoani Rukwa wamemuua kwa kumchoma moto Amosi Kapufi miaka 22 mkazi wa kijiji cha Myunga baada ya kumchoma kisu mtoto wa dada yake aliefahamika kwa jina la Catherin Kakusu na kufariki dunia papo hapo kutokana na wivu wa kimapenzi.
Imedaiwa
kuwa marehemu kabla ya kifo chake alikuwa na mahusiano ya kimapenzi na binti huyo
ambae alikuwa akiishi katika kata jirani
na maeneo anayoishi wilayani humo.
Kwa
mujibu wa mzazi wa kijana huyo, Bosko Kapufi, amebainisha kuwa kabla ya kifo
chake, marehemu alikuwa ameelekea kwenye kata ya Mbuluma kwa lengo la kuwaona ndugu zake, ambapo baada ya kukutana
na binti huyo alianzisha vurugu na
kumchoma kisu binti huyo katika sehemu
za tumbo na shingoni na kufariki dunia.
Amesema
kufuatia tukio hilo wananchi kutoka sehemu mbalimbali walikusanyika kisha kumpiga kijana huyo .
“Kifo
cha kijana wangu kimenisikitisha sana kwani kijana huyu alikuwa mwaka wa kwanza
katika chuo kikuu cha Sauti hivyo sote tumepata hasara kubwa sisi kama wazazi
lakini pia serikali”. Alisema Kapufi
Mkuu
wa wilaya ya Kalambo Julieth Binyura , alikiri wazi kutokea tukio hilo na kusema tukio hilo lilitokea baada
ya watu hao kutofautiana na kuwasihi wananchi kuacha tabia ya kujichukulia sheria mkononi .
“Tukio
hili limetusikitisha sana wananchi wa Kalambo
kwani kitendo cha kufanya mauaji ni kosa, hivyo niwatake wananchi kuacha tabia ya
kujichukulia sheria mkononi na badala
yake kunapotokea tatizo waende kwenye uongozi husika”. Alisisitiza Binyura.
Comments
Post a Comment