MITI YA MIKARATUSI KUKAUKA KUTOKANA NA KUKOSA MADINI YA KORONI - SUMBAWANGA

WAKAZI wa Manispaa ya Sumbawanga mkoani Rukwa wako hatarini kukumbwa na tatizo la ukosefu wa maji 
kutokana miti aina ya mikaratusi iliyopo katika msitu wa Mbizi ambao ni chanzo kikubwa cha maji katika mji huo kuanza kukauka kutokana na ardhi ya eneo la msitu huo kukosa madini ya phosphorus pamoja na boron.

Msitu huo wa Mbizi unaohifadhiwa na wakala wa Misitu Tanzania(TSF) mkoani Rukwa una ukubwa wa hekta 23,427 uko hatarini kutoweka kutokana na miti hiyo kuanza kukauka na ndiyo miti iliyo mingi katika msitu huo.

Meneja wa wakala wa TFS wilayani Sumbawanga,Lucas Kivuyo alisema kuwa baada ya kuona changamoto hiyo walitoa taarifa Kwenye  tasisi ya TAFORI ambapo walifika wataalamu wakiwa na watafiti kutoka chuo kikuu cha kilimo cha SUA ambapo walishauri kupanda miti aina ya mipaini ambao huenda ikastawi katika eneo hilo na hivyo kuondoa hofu ya kutoweka kwa msitu huo ambao ndio chanzo kikuu cha maji kinachotegemewa na wakazi wa Manispaa ya Sumbawanga.

Hata hivyo wataalamu hao walichukua sampuli ya udongo uliopo katika eneo la msitu huo ili kwenda kuufanyia uchunguzi ili waweze kubaini tatizo hasa linalosababisha changamoto hiyo ili waweze kutoa suluhisho la kudumu la tatizo hilo lengo ikiwa ni kuunusuru msitu wa Mbizi ambao ni tegemeo kubwa kwa chanzo cha maji kwa wakazi wa mji wa Sumbawanga.

Awali akizungumzia wakati akiutembelea msitu huo,kaimu  mkurugenzi  mkuu wa taasisi  hiyo ya TAFORI,Revocatus Mushumbusi , alisema kuwa miti hiyo inakabiliwa na ukofu  wa  madini ya Phosporus  na boron ambayo ni muhimu  katika urutubishaji wa miti  hiyo.
Aliwashauri wananchi wa Manispaa ya Sumbawanga kwa kushirikana na wataamu wakati wa kupanda miti ili kuepukana na chanagamoto Kama  hiyo kwani ni vizuri wakatambua ni aina gani ya udongo uliopo na ni miti gani itakubali katika eneo husika.
Pia Mushumbushi aliwashauri wananchi kuacha tabia ya kukata miti hovyo pamoja na kuchoma Misitu hovyo kwani madhara yanayotokana na vitendo hivyo ni makubwa sana na yanachukua muda mrefu kukabiliana nayo.

Comments