
Samatta amejiunga na Aston Villa ya England mwezi uliopita na tayari ameshafunga goli moja baada ya kucheza mechi mbili.
Hata hivyo, kwa siku kadhaa sasa, baadhi ya mashabiki wa mchezaji huyo nchini Tanzania wamekuwa wakishutumu baadhi ya wachezaji wa Villa kuwa ni wachoyo na hawampi pasi Samatta.
Mashabiki hao wamekuwa wakijadili hayo mitandaoni na wengine kuandika malalamiko yao kwenye kurasa rasmi za mitandao ya kijamii ya klabu ya Villa.
Hali hiyo imemlazimu hii leo Samatta kutoa ujumbe kwa maashabiki zake pia kup
"Mashabiki wa soka Tanzania nafahamu kuwa mnanipenda kijana wenu na mnapenda nifanye vizuri katika timu yangu mpya, lakini nawaomba muache kutoa maneno ya kashfa au yenye mrengo mbaya katika kurasa za timu au wachezaji, binafsi sifurahishwi," ameeleza Samatta.
Mashabiki wa Tanzania 'wanamtuhumu' zaidi kwa uchoyo wa pasi kiungo na nahodha wa klabu hiyo Jack Grealish.
Tuhuma hizo zimepamba moto baada ya mechi ya Ligi ya Primia ya baina ya Bournamouth na Villa siku ya Jumamosi.

Villa ilipoteza mchezo huo kwa magoli 2-1. Huku bao pekee la Villa likifungwa na Samatta dakika ya 70.
Kwa mujibu wa baadhi ya mashabiki, Samatta hakutengenezewa nafasi za kutosha na wachezaji wenzake kwenye mchezo huo.
Comments
Post a Comment