Wananchi
mkoani Rukwa wameiomba serikali kuweka
utaratibu maalumu ambao utawawezesha kutoa ushahidi mahakamani kwa kujirekodi
na kutuma video pamoja na vinasa sauti mahakani badala ya kuapa kwa lengo la
kusadia watu kupata haka zao kwa wakati.
Wakiongea
wakati wa maadhimisho ya siku ya sheria yaliyofanyika wilayani Kalambo, walisema serikali haina budi
kuziwezesha mahakama kwa kuruhusu
watu kutuma video
pamoja na vinasa sauti na
kutumika kama ushahidi wakati wa
uendeshaji kesi mahakamani.
Hakimu
wa mahakama ya wilaya ya Kalambo Ramadhani Rugemalira ambae alikuwa mgeni rasm
kwenye madhimisho hayo, alisema kwa sasa
mashauri yote yatatumwa kwa njia ya
simu.
‘’katika
kupunguza gharama za mashauri kwa wadau ,mahakama imeanzisha huduma ya mahakama
inayotembelea {mobile court }alisema Rugemalila.
Alisema
hali kadhalika kwa sasa mahakama inatumia mitambo
ya kielektroiniki {viedo
conferece facility }kuendesha mashauri
mbalimbali kwa baadhi ya
maeneo hapa nchini.
Alisema
mahakama
ya Tanzania katika
kuhakikisha mashauri ya
biashara na uwekezaji yanaisha kwa
haraka ,msisitizo mkubwa umewekwa
kwenye utatuzi wa mashauri kwanjia ya
usuluhishi {Altenative dispute
resolusion }
Alisema
kwa
upande wa mahakama
ya mwanzo mashauri
yatatakiwa kumalizika ndani
ya miezi sita
,mahakama za hakimu mkazi miezi kumi na
mbili kwa mwaka
mara moja .
Mkuu
wa
wilaya ya kalambo Julieth Binyura aliwataka wananchi kujenga mazoea
ya kufika mahakamani kutoa
ushahidi.
‘’wananchi
pia ni
wadau muhimu katika
kuhakikisha kunakuwepo
namazingira wezeshi ya biashara
na uwekezaji.kunapokuwa na shauri lolote
mahakamani zikiwemo kesi za biashara na uwekezaji
ni jukumu la wananchi kufika
mahakani kutoa ushahidi ili
kesi ziweze kufikia maamuzi sahihi na ya haki kwa wakati.’’Alisema Binyura.
Madhimisho
ya
sheria hufanyika tarehe 6 ya
kila mwaka na kwa
mwaka huu yalikuwa na kauli
mbiu isemayo‘’Uwekezaji na biashara,Wajibu wa
mahakama na wadau kuweka mazingira wezeshi ya uwekezaji’’
Comments
Post a Comment