Kenya yaomboleza kifo cha Rais mstaafu

  1. Je, Wakenya watamkumbuka vipi Moi


  2. Je, Moi alikuwa mwanasiasa wa namna gani?

    Kwa zaidi ya robo karne Daniel arap Moi alitawala siasa za Kenya.
    Yeye alikuwa mwanasiasa aliyetaka kupendwa zaidi na wananchi kuliko alivyokuwa mtangulizi wake, rais wa kwanza wa jamuhuri ya Kenya Mzee Jomo Kenyatta.
    Hata hivyo alishindwa kuvunjilia mbali utawala wa kiimla wa Jomo Kenyatta na badala yake yeye mwenyewe akajikuta katika hali ya kuwadhulumu wapinzani wake wa kisiasa.
    Alibatizwa jina la "Profesa wa Siasa" kwa vile alivyoweza kukabiliana na wapinzani wake. Hata hivyo utawala wake ulimalizika na sifa mbaya kwa kuwa Serikali yake ilidumaza uchumi na ufisadi ukashamiri.
    Moi
  3. Rais Msaafu wa Kenya Daniel Arap Moi afariki dunia

    Rais Mstaafu wa Kenya Daniel Arap Moi afariki dunia akiwa na miaka 95, rais Uhuru Kenyatta athibitisha.
    "Kwa masikitiko makubwa natangaza kifo cha kiongozi mkubwa Afrika, Daniel Toroitich arap Moi, rais wa pili wa Kenya. Raisi mstaafu amefariki katika Hospitali ya Nairobi mapema asubuhi ya leo Februari 4 akiwa na familia yake," ameeleza rais Kenyatta.
    Kwa mujibu wa msemaji wa Mzee Moi, Lee Njiru, mipango ya mazishi ya kiongozi huyo kwa sasa yapo chini ya jeshi la nchi hiyo.
    Moi

Comments