NAIBU
waziri wa wizara ya tawala za mikoa na serikali za mitaa(TAMISEM),Josephat
Kandege amewaagiza maofisa watendaji wa serikali waliopo kata ya Samazi
wilayani Kalambo mkoani Rukwa kuwachukulia hatua za kisheria baadhi ya mafundi
wanaodaiwa kukwamisha ujenzi wa kituo cha afya Samazi kilichopo wilayani
Kalambo.
Agizo hilo
alilitoa mwishoni mwa wiki wakati alipokuwa katika ziara ya kikazi na
kutembelea eneo ambalo ujenzi wa kituo hicho unafanyika na kupewa taarifa kuwa
kuna baadhi ya mafundi wamekuwa kikwazo cha maendeleo ya ujenzi wa kituo hicho
cha afya kwa kugoma kufanya kazi kwa madai kuwa fedha wanazopata kutokana na
malipo ya kazi hiyo ni kidogo.
Naibu
waziri huyo,Kandege ambaye pia ni mbunge wa Jimbo hilo la Kalambo alisema kuwa
tayari wananchi wa jimbo hilo wamekwisha kubaliana kuwa yeyote atakaye kwamisha
ujenzi wa kituo hicho cha afya nilazima achukuliwe hatua,ikiwa ni pamoja na
kufikishwa mahakamani kwani hata sheria zinaruhusu kufanya hivyo.
Alisema
kuwa ni vizuri kila mwananchi akashiriki kikamilifu katika ujenzi huo wa kituo
cha afya kwani kutatatua changamoto zinazo wakabiri za kutembea umbali mrefu
kwaajili ya kutafuta huduma za afya.
Kwaupande
wake mhandisi wa Halmashauri hiyo,Daud Sebiga alisema kuwa ujenzi wa kituo
hicho cha afya cha Kata ya Samazi kinatarajiwa kukamilika ndani ya siku 90.
Alisema
kuwa mpaka hivi sasa Halmashauri ya wilaya ya Kalambo imekwisha pokea fedha
kiasi cha shilingi milioni 400 kutoka serikali kuu ambazo zitatumika
kukamilisha ujenzi ndani ya siku 90 wa majengo matatu ambayo yatatumika katika
kituo hicho cha afya.
Naye Juma
Kibongwe diwani wa Kata ya Samazi aliishukuru serikali kwaniaba ya wananchi wa
kata hiyo kwa kutoa fedha hizo ambapo ujenzi wa kituo hicho cha afya utakapo
kuwa umekamilika utawaondolea kero wanazokutana nazo pindi wanapokuwa wagojwa.
Ujenzi wa
kituo cha afya Samazi uilitakiwa kunza June
2019 baada ya serikali kutoa shilingi milioni 400 kwaajili ya ujenzi huo,lakini
umekuwa ukisua sua kutokana na kuibuka kwa mvutano wa eneo gani kijengwe na
kukubalina kujenga katika
eneo la zahanati .
Comments
Post a Comment