Maelfu ya Wakenya na viongozi tofauti wahudhuria ibada ya mazishi katika uwanja wa Nyayo Nairobi

Msafara wa jeneza lake ulienda hadi katika Ikulu ya rais.

watu katika uwanja wa nyayo

Msafara huo baadaye uliondoka katika ikulu ya rais na kuelekea hadi uwanja wa Nyayo mwendo was saa tatu asubuhi ambapo Wakenya walisubiri kuwasili kwa mwili wake kabla ya ibada hiyo.
Tayari baadhi ya viongozi waliowasili ni pamoja na rais wa Rwanda Paul Kagame, Salva kiir wa Sudan na rais Museveni wa Uganda

Wanajeshi

Kuanzia mapema ya saa kumi na moja alfajiri , watu walikuwa wamepanga milolongo mirefu kuingia katika uwanja huo.
Mabasi ya shule kutoka maeneo mbalimbali yaliotumika kubebba kusafirisha watu hadi katika uwanja huo , yaliegeshwa katika maeneo tofauti ya mji huku watu wakiwatakiwa kushuka na kupanga foleni karibu na barabara ya Bunyala.
Viongozi wengine waliowasili kwa ibada hiyi ya kitaifa ni marais wa zamani wa Tanzania Benjamin Mkapa na Jakaya Kikwete.
Mwili wake kwa sasa unazungushwa ndani ya uwanja huo polepole na kusindikizwa na wanajeshi kutoka jeshi la Kenya.
Mwili wake uliopo ndani ya jeneza unabebwa na gari maalum na nyuma ya gari hilo kuna gari jingine ambalo limewabeba watoto wa kiongozi huyo akiwemo mwanwe wa kike June Moi, Raymond Moi ambaye ni mbunge wa Rongai , na Gideo Moi seneta wa Baringo.

Mwili wa rais mstaafu Daniel Moi ukizungushwa katika uwanja

Takriban viongozi 12 wakiwemo marais wa zamani wanahudhuria hafla hiyo
Rais Uhuru Uhuru Kenyatta na mkewe Margaret Kenyatta waliwasili katika uwanja wa Nyayo kwa ibada ya mazishi ya kiataifa ya rais mstaafu Moi mwendo wa saa tatu.
Uhuru Kenyatta analiongoza taifa katika ibada hiyo.

Uwanja wa Nyayo

Wiki iliopita , serikali ilitangaza siku ya Jumanne kuwa sikukuu ya ili kuwafanya Wakenya wengi kuhudhuria ibada hiyo. Mwili wa Moi ulikuwa bungeni ambapo takriban raia 213,000 waliruhusiwa kuuona kulingana na maafisa wa polisi.
Mazishi ya kitaifa yam zee Moi yatakuwa ya pili kufanyika nchini huku raia na wanjeshi wakitoa heshima zao baada yay ale ya mwanzilishi wa taifa la Kenya Mzee Jomo Kenyatta.

Baadhi ya raia kutoka jamii ya Masai wakisikiliza kwa makini hotuba zilizokuwa zikitolewa
Image captionBaadhi ya raia kutoka jamii ya Masai wakisikiliza kwa makini hotuba zilizokuwa zikitolewa

Hafla hhiyo ya kutoa heshima inashirikisha kutoa hshima kwa kubeba mwili wake katika gari maalum lililosindikizwa na wanajeshi waliobeba bunduki pamoja na ngoma za kijeshi ikiwemo ufyatuaji wa risasi 19.
Tofauti na maishi ya mtangulizi wake ni kwamba huku Mzee Moi akipigiwa risasi 19 na kwamba hatovalishwa magwanda ya kijeshi , Mzee Kenyatta aliyefariki akiwa afisini 1978 na alikuwa amevalia nguo za kijeshi..

Comments