Serikali Yatoa Dawa Za Mifugo . Wafugaji Waipongeza Serikali.



SERIKALI imeanzisha kampeni maalumu ya kupambana na magonjwa ya mifugo kwa kusambaza dawa katika majosho yote ikiwa ni jitihada za kuwasaidia wafugaji ili kuondokana na changamoto ya kufa kwa mifugo yao.

Ofisa mifugo mfawawidhi wa kituo cha uchunguzi wa magonjwa ya  mifugo kanda  ya  kusini magharibi Dkt Kaini Kamwela,alisema kuwa huo ni mkakati wa serikali katika kuhakikisha wafugaji wanafuga mifugo yao kitaalamu na kuondokana na adha  ya  kufa kwa  mifugo yao.

Alisema kwa muda mrefu  wafugaji wamekuwa  wakikutana na chanagamoto ya kushindwa kuongesha mifugo kutokana na ukosefu wa dawa pamoja na gharama   ya kuongeshea mifugo kuwa kubwa.
Alisema kwa kutambua hilo serikali  imepunguza gharama za kuongeshea mifugo kwa asilimia mia moja.
Aliyasema hayo mara  baada ya kutembelea josho la kuogeshea mifugo  lililopo katika kijiji cha Kate wilayani Nkasi mkoani  Rukwa.
Baadhi ya wafugaji katika kijiji hicho waliipongeza serikali  kwa  jitihada  hizo na kusema kuwa awali walikuwa wakiogesha mifugo kwa bei kubwa na hivyo  kusababisha  kushindwa  kumudu  gharama sambamba na matibabu kuwa bei juu.
"tunaishukuru sana serikali  kwa  jitihada zake katika  kuwapatia  dawa za mifugo pamoja na kuongeza idadi ya mashojo kwani hatua hiyo itawawezesha kuondokana na changamoto ya kufa  kwa  mifugo yetu’’ walisema wafugaji  hao.


Comments