Eneo la machinjio ya nyama |
Na Baraka lusajo. Rukwa.
WAKAZI wa manispaa ya Sumbawanga
mkoani Rukwa wamelalamikia kufungwa ghafla kwa muda usiojulikana
machinjio ya mifugo ya Manispaa hiyo kitendo kitakacho sababisha
kukosekana kwa kitoweo cha nyama katika mji huo.
ENEO LA MACHINJIO |
Wakizungumza kwa nyakati tofauti
wamesema kuwa machinjio hayo ndiyo yanayotegemewa na wakazi wa
Manispaa hiyo kwa na kufungwa bila kuwa na eneo mbadala kunaweza kusababisha
kukosekana kabisa kwa kitoweo cha nyama, hivyo kuiomba
serikali kuteua eneo mbadala ili kuwawezesha wakazi hao kuendelea
kupata kitoweo kama ilivyo kuwa hapo awali.
Alex mwita ni mmoja wa mkazi wa mji wa
Sumbawanga, alisema kuwa serikali haina budi kuweka utaratibu
maalumu utakao wawezeaha wao kupata kitoweo hicho kwani
walikuwa wamezoea kwenda kununua nyama kwenya machinjio
hayo lakini kufungwa kwake kutafanya kukosa mboga
ya kutumia majumbani.
"Machinjio imefungwa ghafla
sana,nafikiri kwamaoni yangu serikali ingetafuta njia mbadala
ya kutunusuru na suala hili kwani hatuelewi
tutapata wapi tena kitoweo cha nyama kutokana na kuwa
awali tulikuwa tukitegemea hapa’’ alisema.
KATIKA PICHA NI KAIMU MSAJILI WA BODI YA NYAMA NCHINI |
Awali akiongea na wachinjaji
mifugo pamoja na wananchi, Kaimu msajili wa bodi ya nyama
nchini,Imani Sichwale, amesema kuwa kalo hiyo ya mifugo haina vigezo vya
kuhifadhia nyama na kusema kuanzia sasa inafungwa rasmi.
‘’kalo hii haina vigezo na
kibaya zaidi imejengwa katikati ya mji
hivyo kuanzia leo imefungwa na mkurugezi atawatafutia njia
mbadala.’’alisema
Alisema kwa kawaida nyama
haitakiwi kugusa chini wala kuchinja mifugo
ikiwa chini kwani kwa kufanya hivyo
kunafanya walaji wa nyama kula nyama chafu.
Alisema kuwa Manispaa kutumia kalo
kama machinjio ni kosa na kusema kuwa suala hilo atalipeleka
kwa mkurugezi ili awatafutie wachinjaji sehemu mbadala ya kuchinjia
mifugo yao.
Comments
Post a Comment