Katika picha ni baadhi ya maafisa elimu pamoja na walimu. |
Mkuu wa mkoa wa Rukwa ,Joachim Wangabo ametoa mwezi mmoja kwa wakuu wa wilaya wa mkoa huo wahakikishe shule zote za msingi na sekondari zinaanzisha klabu za wapinga Rushwa lengo ni kuwawezesha wanafunzi kuwa wadilifu na viongozi bora wa badaye.
Akiongea kwa niaba ya mkuu wa
mkoa huo, mkuu wa wilaya ya Sumbawanga Dkt, Halfan Haule wakati akifungua mafunzo
ya kuwajengea uwezo wa kukabiliana na rushwa walimu wa shule za msingi na
sekondari pamoja na maafisa elimu mkoani humo,alisema lengo la serikali ni
kutokomeza kabisa vitendo vya rushwa.
mwakilishi wa mkuu wa mkoa wa Rukwa |
"kupitia hadhara hii
ningependa kutoa wito kwa wakuu wa wilaya zote katika mkoa kuhakikisha kila
shule ya sekondari na msingi katika wilaya husika inakuwa na klabu
ya wapinga Rushwa na taarifa ya utekelezaji niipate kabla au ifikapo
mwishoni mwa mwezi februari" alisema.
katika picha ni maafisa elimu |
Alisema kuwa katibu tawala wa
mkoa ahakikishe maelekezo haya yanawafikia wakuu wa wilaya kwa barua
rasmi na nakala ya barua niione kwenye jalada.
Alisema ili watoto na vijana
wawe viongozi bora na wadilifu ,ni lazima malezi yaanzie ngazi ya familia
na kuendelezwa shuleni hasa shule za awali , msingi na sekondari.
Mkuu wa TAKUKURU mkoni humo,Hamza Mwenda, alisema
Rushwa ni uozo wa kimaadili.
"maadili ni siraha
muhimu katika mapambano dhidi ya rushwa kutokana na ukweli kwamba rushwa
ni uozo wa kimaadili na maadili kwa maana ya mwenendo mwema hujengwa ndani ya mtu
tangu anapozaliwa alisema Mwenda.
Hata hivyo
mafunzo hayo yameshirikisha walimu walezi wa shule za
msingi na sekondari pamoja na maafisa
elimu katika shule zote za
Comments
Post a Comment