KATIKA NI BAADHI YA WANANCHI WALIOKOSA MAKAZI |
KAYA 47 zimebaki bila makazi baada ya nyumba 13 kubomoka
kutokana na mvua kubwa iliyonyesha juzi katika kijiji cha kasitu kata ya sopa
wilayani kalambo mkoani Rukwa.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti baada ya tukio hilo
kutokea ,wakazi wa kijiji hicho walisema kuwa mvua hiyo ilikuwa kubwa na
imeambatana na upepo mkali ilianza kunyesha majira ya saa nane na dakika
arobaini na tano mchana na
kusababisha kubomoka nyumba hizo.
Anold Yolam,mkazi wa kijiji hicho alisema kuwa
baadhi ya watu ambao nyumba zao zimebomoka wamepewa hifadhi kwa
mwenyekiti wa serikali ya kijiji na wengine wamepewa
hifadhi kwa majirani na kuiomba serikali iwasaidie.
Naye Jeriko Malema alisema kuwa mvua hiyo ilinyesha kwa
muda mfupi lakini iliambatana na upepo mkali na hali
itasababisha kubomoka kwa nyumba hizo.
Kwaupande wake ofisa mtendaji wa kijiji hicho Gasper Kateka
alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema kuwa nyumba 13 zimeanguka na
kuwaacha watu 47 bila makazi.
Alisema kuwa baadhi ya wananchi ambao nyumba zao zimebomoka
wamepewa hifadhi kwa mwenyekiti wa kijiji na wengine
kwa majirani wakati wakisubiri msaada zaidi.
Mwenyekiti wa kijiji hicho John Sizo
alisema kuwa wananchi wengine ambao hawakupatwa na janga hilo wanawajibu wa
kuwasaidia watu waliopatwa na maafa hayo.
Mkuu wa wilaya ya Kalambo Julieth Binyura, alisema tukio hilo limetokana na wananchi kutojenga nyumba imara na
zenye ubora kwani ndizo zitakazo saidia kuondokana na adha hiyo.
Alisema nyumba nyingi zilizo athirika hazikuwa zimejengwa kwa
kufuata taratibu za ujenzi bora hivyo wananchi wanapaswa kuwashirikisha wataamu
wa halmashauri pindi wanapo jenga nyumba zao ili wawape
ushauri wa namna ya kujenga nyumba bora.
Comments
Post a Comment