| kushoto ni mkuu wa wilaya ya Kalambo akiungana na wananchi katika kupima afya katika kituo cha afya Matai |
Na Baraka Lusajo.Kalambo.
Halmashauri ya Wilaya ya
Kalambo mkoani Rukwa imeanzisha utaratibu maalum wa kuwasaidia wananchi kwa
kusambaza Madaktari Bingwa katika vituo mbalimbali vya afya lengo ikiwa ni
kuondokana na changamoto ya kutembea umbali mrefu kwaajili ya kutafuta
matibabu.
| katika picha ni mkuu wa wilaya akipima afya na mganga mkuu wa wilaya hiyo Aleni Mlekwa ikiwa ni jitihada za kuhamasisha wananchi kujitokeza kujua afya zao. |
Mganga Mkuu wa Wilaya hiyo
Aleni Mlekwa alisema kuwa madaktari hao wamesambazwa katika vituo vyote vya
afya wilayani humo ambavyo ni kituo cha afya cha Mwimbi, Matai na
Ngorotwa.
Alisema kuwa lengo ni
kuwezesha wananchi kuondokana na adha ya kutembea umbali mrefu kwaajili
ya kufuata huduma za matibabu.
Madaktari hao
walichukuliwa kutoka hospitali ya mkoa wa Rukwa na wananchi elfu mbili
wamekwishatibiwa na zoezi hilo bado linaendelea.
Alisema kutokana na
mwitikio wa watu kuwa mzuri wameongea na uongozi wa Wilaya ili
katika awamu ijayo bajeti iongozwe kwa lengo la kufikisha huduma
hiyo katika zahanati zote za wilaya hiyo.
"Katika zoezi hili
tuna madaktari wa aina mbalimbali ikiwemo wa Macho, Madaktari wa
magonjwa ya ndani, madaktari wa magonjwa ya akina mama, Madaktari wa
magonjwa ya watoto pamoja na Madaktari wa upasuaji na
tunaishukuru sana serikali kwa kutoa
fedha ili kuwasaidia wananchi wanaoishi katika
maeneo ambayo hayafikiki kiurahisi,"Alisema Mlekwa.
Mmoja wa Madaktari
bingwa mkoni humo,Hamisi Ulaya alisema mwitikio wa
wananchi umekuwa mzuri kwani kila sehemu waliyopita watu
walikuwa na uhitaji wa kutibiwa.
Mkuu wa wilaya ya Kalambo
Bi. Julieth Binyura, aliwasihi wananchi wilayani humo
kuendelea kujitokeza kwa wingi kwenye zoezi hilo ili
kupata matibabu katika maeneo hayo.
Alisema lengo la Serikali
ya awamu ya tano ni kuhakikisha wananchi wanaondokana na
adha ya kutembea umbali mrefu kutafuta huduma za matibabu na
kuwataka wahudumU wa afya kutoa vitambulisho
kwa wazee wote.
| katika picha ni baadhi ya wananchi waliojitokeza kipima afya zao katika kituo cha afya cha Mwimbi. |
Baadhi ya
wananchi wilayani humo wameipongeza Serikali kwa kusogeza
huduma za matibabu karibu na maeneo yao na
kuomba kuwa na utaratibu maalumu wa kurudiwa
kwa zoezi hilo.
Comments
Post a Comment