KATIKA PICHA KULIA NI MKUU WA MKOA AKIWA ANAWALEKEZA WAKULIMA |
Na Baraka Lusajo. Kalambo.
Wakulima mkoani Rukwa wamelalamikia kukosekana kwa pembejeo
pamoja na bei elekezi katika msimu huu wa kilimo hali inayotia hofu kutopata
mavuno makubwa kutokana na wakulima
wengi kulima bila kutumia pembejeo na kuiomba
Serikali kuweka utaratubu maalumu wa kusambaza pembejeo kabla ya msimu kuanza.
Wakiongea wakati wa uzinduzi wa baadhi ya mashamba katika kijiji cha Kalalasi Wilayani Kalambo yaliozinduliwa
na Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mhe. Joachim
Wangabo.
KATIKA PICHA NI MKUU WA WILAYA YA KALAMBO JULIETH BINYURA AKIPANDA MBEGE ZA MAHINDI KATIKA SHAMBA LA MKULIMA. |
Walisema wamekuwa wakikabiliwa na changamotoya kucheleweshewa kwa pembejeo za kilimo na kuwalazimu kutumia
pembejeo ambazo si bora.
Walisema serikali haina budi kuweka utaratibu maalumu ambao
utawawezesha kupata pembejeo mapema kabla ya msimu kuanza .
‘’Tunaiomba Serikali kuanzisha utaratibu mzuri ambao utatuwezesha
kupata pembejeo mapema kwani kila mwaka pembejeo
hususani mbolea na mbegu zimekuwa
zikiletwa kwa kuchelewa sana.”
KATIKA PICHA NI KATIBU TAWALA FRANK SICHALWE AKILIMA NA NYUMBA YAKE NI MKURUGEZI WA HALMASHAURI YA KALAMBO MSONGOLA PALELA . |
Aidha, waliipongeza serikali mkoani humo kwa kuweka utaratibu wa kuwatembelea mashambani na kuwa utaratibu huo
utawasaidia kwa kiasi kikubwa
kuhamasika na kulima kilimo bora
na chenye tija.
Afisa kilimo Mkoani humo Ocran Chengula, alisema pembejeo za
kilimo zipo za kutosha na kusema shida ni wakulima wengi kuwa na mazoea ya kununua pembeo pindi msimu
wa kilimo unapoanza.
‘’Pembejeo zipo za kutosha, tatizo ni kwamba wakulima
wengi wamezoea kununua
pembejeo wakati msimu unapoanza ilihali kwenye
maduka na maghara ya pembejeo katika
misimu yote zinakuwa zipo, hivyo
wakulima mjipange mnaweza kununua pembejeo muda na wakati wote
badala ya kusubiri kuanza kwa msimu, alisema Chengula.
Awali akikagua mashamba
ya wakulima Wilayani Kalambo, Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mhe. Joachim Wangabo,
aliwasihi wakulima kulima kilimo chenye
tija na ambacho kitawasaidia
kujikwamua na hali ya kiuchumi.
Alisema kila mkulima anawajibu
wa kuwatumia wataalamu
wa kilimo kwenye maeneo husika
ikiwa ni pamoja na kutumia mbolea
na viuatiulifu kwa lengo la
kupata mavuno mengi.
‘’Endapo tukifanya hivyo
tutaweza kufikia malengo
yetu ya kimkoa
ambapo mwaka jana tulikuwa na
tani laki nne na tisini na
nne na mwaka huu
tunataka kufikia tani laki saba za
mahindi peke yake, lakini tutaweza kufikia kiwango
hicho endapo tutalima kilimo chenye tija.” Alisema Wangabo.
Comments
Post a Comment