KULIA NI MKUU WA MKOA WA RUKWA AKIONGEA NA WAKULIMA KATIKA BONDE LA ZIWA RUKWA |
Wakulima wa zao la
alizeti katika bonde la ziwa Rukwa wilaya ya Sumbawanga mkoani Rukwa
wameiomba serikali kuweka bei elekelezi kwenye mbegu ya zao hilo
kutokana na gharama kuwa juu
hivi sasa hali inayosababisha baadhi yao kushindwa kulima zao hilo.
Wakiongea kwa
nyakati tofauti wakati wa mandalizi ya zao hilo kwenye
mashamba yao ,wamesema kuwa changamoto kubwa ni ukosefu wa
masoko na bei ya mbegu kuwa kubwa kiasi kwamba wanahofu
baadhi yao watashindwa hata kulima zao hilo katika msimu huu.
Wamesema serikali haina
budi kuweka bei elekezi ya mbegu
ya zao hilo kama ilivyo kwa pembeo nyingine
za kilimo kwa lengo la kuwasaidia kuinua kipato chao.
"tunaiomba serikali
itutafutie masoko ya uhakika kwani kwa huku kwetu
bondeni kuzalisha tunazalisha sana alizeti lakini tatizo
ni wapi utaipeleka"walisema.
Afisa kilimo wilayani
Sumbwanga Joseph Bakuli amesema lengo ni kuwa zao la alizeti kuwa miongoni mwa
mazao ya kimkakati ndani ya mkoa hivyo wananchi wanawajibu wa kulima zao
hilo na kuondokana na kutegemea zao moja la mahindi.
Naye mkuu wa mkoa wa
Rukwa ,Joachim Wangabo, amewataka wananchi
kufuata kanuni bora za kilimo kwa kuwashirikisha
wataamu lengo likiwa ni kufikia mafanikio.
Hata hivyo katika msimu
wa kilimo wa mwaka 2018/2019 jumla ya hekta 66,872.15 za alizeti zililimwa
katika mkoa wa Rukwa na kupatikana tani 61,651.11.
Comments
Post a Comment