Ni matokeo
yaliyotarajiwa, Freeman Mbowe ambaye amekiongoza chama kikuu cha upinzani
Tanzania Chadema kwa miaka 15, amepewa tena ridahaa na wanachama kushikilia
usukani wa chama kwa miaka mitano ijayo.

Upinzani dhidi yake
kwa mwaka huu, kama ilivyokuwa miaka mitano iliyopita ulikuwa ni hafifu,
akishinda uchaguzi huo uliofanyika Jumatano wiki hii alishinda kwa kishindo cha
asilimia 93.5.
Baada ya kutangazwa
mshindi, wafuasi wake kwa furaha wakamuimbia: "...tuvushe mwamba
tuvushe."
Mwamba anayezungumziwa
ni Mbowe, lakini awavushe kutoka wapi na kuelekea wapi ni jambo ambalo kila mtu
anaweza kuwa na tafsiri yake.
Moja ya tafsiri
inaweza kuwa kuwavusha kutoka kwenye changamoto zinazowakumba kwa sasa, na
katika hilo changamoto ni za upinzani kwa ujumla.
Comments
Post a Comment