KATIBUmkuu ofisi ya Rais Tawala za
mikoa na serikali za mitaa(Tamisemi),Joseph Nyamuhanga ametoa siku 90 kwa
halmashauri ya wilaya ya Kalambo mkoani Rukwa kuhakikisha inaanza ujenzi wa kituo cha afya Samazi vinginevyo itanyang'anywa fedha zilizotolewa kwaajili ya
ujenzi wa kituo hicho.
Agizo
hilo alilitoa hivi karibuni alipokuwa katika ziara ya kukagua maendeleo ya
ujezi wa vituo vya afya pamoja na hospitari za wilaya katika mkoa
wa Rukwa.
Alisema
kuwa serikali ilitoa fedha muda mrefu, kiasi cha
shilingi milioni 400 kwaajili ya ujezi wa kituo hicho cha afya lakini
mpaka sasa ujezi wake haujaanza kitendo ambacho ni kuchelewesha huduma kwa
wananchi.
"Serikali
imetoa maelekezo na sio muanze tena marumbano ya wapi kijengwe kituo hicho kama
mtaendelea na hali hii mtanyang'anywa fedha hizo wapewe wengine wanao zihitaji
na wako tayari kutekeleza maelekezo ya serikali kwa wakati" alisema
Aidha
aliekeza kuwa kwakuwa katika Kijiji hicho tayari kuna zahanati ,nibora iliopo ipanuliwe ili kuwe na majengo mengi
ambayo yatakidhi mahitaji ya sasa ambapo ilichopo imeonekana ni ndogo
kutokana na idadi ya watu waliopo wakati huu.
Aidha
alisema kuwa serikali inategemea kutoa fedha kiasi cha shilingi
milioni 300 kwa kila hospitali ya wilaya kwa ajili ya kukamilisha ujenzi
na aliwaagiza wakurugezi nchi nzima kuzitumia fedha hizo vizuri ili
zikidhi mahitaji.
Hata
hivyo imeelezwa kuwa zaidi ya vituo vya afya 350 vipya vimejengwa
nchi nzima na vituo vingine 67 vinatarajiwa kujengwa ifika mwaka
2020.
Comments
Post a Comment