![]() |
Kushoto ni mkurugezi mtendaji Palela Msongela wakiwa mapumziko na katika tawala Frank Sichalwe baada ya kutoka kwenye shughuli ya upandaji miti. |
KATIKA jitihada za kutunza na kuhifadhi Mazingira, Halmashauri ya wilaya ya Kalambo mkoani Rukwa imeanza utaratibu maalumu wa kupanda miti katika maeneo tofauti ya wilaya hiyo na tayari imefanikiwa kupanda miti 1200 katika mji wa Matai.
![]() |
Mmoja wa watumishi akipanda miti katika eneo la halmashauri. |
Kaimu afisa mazingira wilayani humo Majanael Swalehe, alisema zoezi hilo
litakuwa endelevu,ambapo wanatarajia kila jumamosi ya mwisho wa mwezi
watakuwa wanapanda miti katika maeneo mbalimbali ya Halmashauri
hiyo ikiwa ni jitihada za kusaidia kutunza na kulinda mazingira ili
yasiharibike.
"mpaka sasa tumefanikiwa kupanda miti 1200 na ili
kuendeleza jitihada hizo tumeamua kuwa kila jumamosi ya mwisho
wa mwezi tutakua tunaendelea na kampeni hii na mwisho wa
mwezi huu tutapanda miti katika eneo la hospitali ya
wilaya" alisema ,Mjanaeli .
![]() |
Mkurugezi mtendaji wilayani kalambo Msongela Palela akipanda miti |
Hata hivyo siku ya Desember 8 ambayo ilikuwa siku ya
kumbukumbu ya uhuru wa Tanganyika,wilaya ya
kalambo ilitumia siku hiyo kupanda miti kuzunguka
maeneo yote ya ofisi za Halmashauri ambapo
viongozi mbali mbali wa wilaya walijitokeza
kushiriki zoezi hilo.
Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Msongela Palela aliwataka
wananchi kuwa na utaratibu wa kupanda miti katika
maeneo yao ikiwa ni jitihada za kuzia upepo
ili usiharibu makazi yao na huku katibu tawala
wilaya hiyo, Frank Sichalwe aliwapongeza wananchi kwa
kujitokeza kwa wingi katika zoezi hilo.
‘’tunawapongeza wananchi
kwa kujitokeza kwenu lakini ni vizuri mkawa na utaratibu wa
kupanda miti katika maeneo ya makazi yenu ili kuhifadhi na
kutunza mazingira.’’walisemaa viongozi
hao.
Comments
Post a Comment