HABARI ZA HIVI PUNDE. Baadhi Ya Wananchi Walazimika Kuyahama Makazi Yao Kutokana Na Maji Ya Mvua Kujaa Kwenye Kingo Za Nyumba Zao.


Baadhi ya wananchi katika mji wa Kasanga wilayani Kalambo mkoani Rukwa wamelazimika kuyahama makazi yao nyakati za usiku baada ya maji kujaa hadi kufikia usawa madirisha kufuatia mvua kubwa  ilionyesha usiku  wa kuamkia Desember 29,2019.

Kwa mujibu wa afisa tarafa ya Kasanga Endrue Manyema Ngindo , amesema baadhi ya nyumba za kulala wageni pamoja na nyumba za  wananchi ziliweza  kujaa maji na kupelekea kuyahama makazi yao.

‘’baadhi ya nyumba za kulala wageni ikiwemo ya Atupenda ‘’A’’ inayomilikiwa na Rhoda Maseba ilikuwa ndani ya maji usawa wa madirisha na kusabisha wateja wake kuhama usiku huo’’alisema Ngindo.

Aidha aliongeza kwa kusema nyumba ya Dorcas Nakazwe moja ya ukuta wa nyumba yake ulibomoka na kupelekea wapangaji wake  kukimbia  usiku  huo .

Comments