Chifu Azikwa Bila Jeneza Akiwa Amekaa Kwenye Kiti.

KABURI  LA  CHIFU


WANANCHI wa kata ya Mambwekenya Wilayani Kalambo wamejikuta katika sintofahamu baada ya kuzuiliwa kushiriki mazishi ya kiongozi wa baraza la machifu mkoani Rukwa ,chifu Christofa Kutazungwa aliyezikwa bila jeneza huku akiwa amekaa kwenye kiti chake na ngozi ya ng’ombe ikilazwa chini  badala kumzika mtu mzima kama  sadaka.
KAMATI  YA KUCHIMBA NA KUFANYA MAZISHI  YA CHIFU
Wakiongea kwa nyakati tofauti wakati mazishi ya chifu huyo wamesema mazishi ya machifu yamekuwa yakifanyika nyakati za usiku  tofauti na mazishi hayo ambayo yamefanyika  mchana na huku watu wakizuiliwa  kulia na kushiriki kuchimba kaburi pamoja na maziko.
MWILI  WA  CHIFU UKIPELEKWA  MAKABURINI KWA  AJILI  YA  MAZISHI NA HUKU  UKIWA  UZUNGWA NA AKINA MAMA
John Sichula mkazi Kijiji cha Mambwekenya ,alisema kwake tukio hilo limekuwa  la kwanza kuona mtu akizikwa bila jenaza na kusema wamezoa  kushiriki  katika  mazishi ikiwemo kuchimba  makaburi  lakini  imekuwa  tofauti kabisa  na  mazizishi  ya  chifu  huyo.
Alisema licha ya hilo  wamezoea kuona  mazishi  ya machifu yakifanyika  nyakati za  usiku  lakini  imekuwa  tofauti  kwa  kiongozi  huyo  kutokana na kuzikwa muda wa mchana  huku  kila  mtu akiwa  anaona  na hivyo kuonekana ni kitu  kigeni  kwao.
Naye Boidi Sichula mkazi  wa maeneo hayo ,alisema kilicho mshangaza  ni  kuona chifu anazikwa  akiwa  amekaa na ngozi  ya  ng’ombe kutandikwa  chini  na kusema katika  maisha yake yote  hajawahi  kuona kitu kama  hicho.
 Daud Mbaya makazi Wa maeneo hayo,alisema kilicho mshangaza  zaidi nikuona watu wakizuiliwa kushiriki  mazishi  hayo pamoja na kulia wakati  wa  msiba.
‘’tumezoea akina mama wakilia wakati wa msiba lakini imekuwa  tofauti  kwa  kiongozi huyo  kutokana na watu kuzuiliwa  kulia  zaidi ya  kucheza ngoma na kuiomba  nyimbo’’alisema .
kwa upande wake kiongozi anaesimika machifu mkoani humo Richad Sinyangwe,alisema wanazika na ngozi ya ng’ombe ikiwa ni badara ya sadaka ya kumtoa mtu.
Alisema kipindi  cha  nyuma  ilikuwa  ni  lazima  kiongozi  mkubwa  kama  huyo  kuzikwa  na  mtu  aliye  hai lakini  badae  walikaa na kufanya  maboresho na kuanza  kutumia ngozi  ya mnyama pamoja na damu ya mnyama  kama ishara ya sadaka.
Alisema  kufanya hivyo kuna onyesha kuwa sadaka inapokelewa na mizimu na kusema hakuna  madhara yoyote  yanayoweza  kutokea .
MACHIFU  WALIO HUDHULIA  KWENYE  MSIBA HUO
Kwa  upande  wake chifu Ntono wa  nne wa  himaya  ya  Ulungu Maiko  Sikazwe ,alisema chifu huyo amezikwa na ngozi na akiwa amekaa lengo ikiwa  ni  kudumumisha mila ya  kichifu.

Mwakilishi wa mkuu wa mkoa huo, Julieth  Binyura ambayepia ni mkuu wa wilaya ya Kalambo,alisemac hifu huyo ndie aliyekuwa kiongozi mkuu wa machifu  mkoani humo na kifo chake kimewachia simanzi  kubwa kutokana na uadilifu  aliokuwa nao  enzi za uhai wake.
Aidha aliwataka  wananchi kuendelea kufanya kazi kwa bidii ikiwa ni ishara  ya  kumuenzi kiongozi huyo ambaye alikuwa mchapakazi mzuri na kuwa  mfano  wa  kuigwa.


Comments