Uongozi
wa Halmashauriya wilaya ya Kalambo Mkoani Rukwa umesema hautasita kuwachukulia
hatua kali za kisheria ikiwemo kuwafikisha mahakamani watendaji wote wa vijiji
na kata ambao watashindwa kuwasilisha fedha benki za mapato ya ndani na kukaa
nazo majumbani kinyume na utaratibu.
Akiongea
kupitia mwendelezo wa vikao kazi vilivyofanyika katika tarafa za Ulumi na Mambwenkoswe,Katibu Tawala wilayani
humo,Frank Sichalwe, amesema baadhi ya watendaji wamekuwa wakikyuka madili yao
ya kazi na kutumia fedha katika matumizi
yao binafusi.
‘’acheni mtindo wa kukaa na fedha za makusanyo majumbani mwenu, baada ya uchaguzi tutaanza kukagua mtendaji mmoja baada ya mwingine na atakae bainka
atachukuliwa hatua kali za kisheria.alisisitiza sichalwe.
Comments
Post a Comment