Wasimamizi Wa Vituo Vya Uchaguzi Waonywa Vikali


        
katika picha ni msimamizi  msaidi  wa uchaguzi  jimbo  la Kalambo Kanoti Mbawala akiongea  na wasimamizi  wa uchaguzi ngazi  ya vijiji  ,kata  na vitongoji.


Na Baraka Lusajo. Kalambo.


UONGOZI wa Halmashauri ya wilaya ya Kalambo mkoani Rukwa umewaonya watendaji pamoja na wasimamizi wa uchaguzi utakao fanyika kesho kutojihusisha na vitendo vya udanganyifu vinginevyo watachukuliwa hatua kali za kisheria.
Onyo hilo limetolewa jana na msimamizi msaidizi  wa uchaguzi wa wilayani hiyo Mbawala  Kanoti katika kikao kazi kilicho fanyika katika ukumbi wa Halmashauri  hiyo.
Alisema kuwa mara kwa mara wasimamizi wa uchaguzi katika vituo vya kupigia kura ndiyo wamekuwa wakisababisha wananchi kutokuwa na imani na matokeo kutokana na baadhi yao kukiuka madili yao ya kazi kwa kuchukua hongo kutoka kwa wagombea.
Alisema kuwa kufanya kazi kinyume taratibu kumekuwa kukisababisha malalamiko hivyo kuwataka kujiepusha na vitendo hivyo ili kufanya uchaguzi huo kuwa wa amani.
"uzoefu unaonyesha sisi watendaji wa serikali ndio tumekuwa vinara kwani tumekuwatu kisababisha kuibuka malalamiko kutoka kwa wa pigakura ,pia lazima  mkumbuke kuwa vyombo vya sheria havita wavumilia endapo mtakwenda kinyume na utaratibu'’alisema
Alisema kuwa katika  uchaguzi huo vitongoji 78,vijiji 33 na kata 14, ndio  vitashiriki  katika uchaguzi huo.
Msimamizi huyo wa wilaya alisema  kuwa katika wilaya hiyo jumla ya vijiji 78, vitongoji  na kata 344  hakutakuwa na uchaguzi  kutokana na wagombea wa baadhi ya vyama pinziani kujitoa  na wengine kuondolewa kutokana na kuwekewa pingamizi hali inayotoa fursa kwa wagombea wa Chama cha Mapinduzi kupita bila kupingwa.
katika picha ni baadhi  ya  wasimamizi  wa vituo  vya  uchaguzi
Alisema kuwa uchaguzi  utaanza majira ya  saa 2:00 za asubuhi  na   kuhitimishwa  saa 10:00 za jioni  na aliwataka wananchi kujitokeza kwa wingi  kupiga  kura kwa lengo la  kuchagua viongozi  bora  na ambao  watakuwa masaada katika maeneo yao na taifa  kwa ujumla.
Kwaupande wao watendaji pamoja na wasimamizi hao walisema kuwa wamejipanga vizuri ili  kuhakikisha uchaguzi unafanyika kwa amani na utulivu na wanaimani kuwa hakutakuwa na malalamiko kwakua taratibu zote zitafuatwa.

Comments