RC Wangabo Aviagiza Vyombo Vya Dola Kumsaka Na Kumkamata Mkadarasi Anajenga Barabara Ya Mji Wa Matai.
Katika picha ni mkuu wa mkoa wa Rukwa Joachm Wangabo. |
MKUU wa mkoa wa Rukwa Joachim Wangabo ameiagiza tasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa (TAKUKURU) kumsaka na kumkamata mkandarasi wa kampuni ya Grand Tech LTD ya jijini Dar es salaam inayotengeneza barabara ya Lami yenye urefu wa kilometa mbili katika mji wa Matai wilayani Kalambo kwa tuhuma za kulipwa fedha zaidi ya nusu ya kazi kisha kuitelekeza.
Agizo hilo alilitoa jana katika kikao cha bodi
ya barabara ya mkoa huo kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ofisi ya
mkuu wa mkoa huo.
wajumbe wa kikao |
Mkuu huyo wa mkoa ambaye pia ni mwenyekiti wa
kikao cha bodi hiyo alitoa agizo hilo baada ya kupokea malalamiko kutoka kwa
mkuu wa wilaya ya Kalambo Julieth Binyura aliyelalamikia mkandarasi huyo
kulipwa fedha kiasi cha shilingi milioni 544.2 sawa na asilimia 67 ya fedha
yote ya mradi huo ambayo ni shilingi milioni 899.7 na kisha kuitelekeza kazi
hiyo.
Alisema kuwa kwa mujibu wa mkataba wa
mkandarasi huyo alipaswa kuwa ameisha kamilisha ujenzi wa kipande hicho cha
barabara na kufikia Novemba 2 lakini bado na mpaka sasa yupo kwenye muda wa
makato kutokana na kuchelewesha kazi hiyo.
Mkuu huyo wa mkoa aliiagiza takukuru kufikia
siku ya jumatatu wiki ijayo ni lazima mkandarasi huyo awe amefikishwa mkoani
Rukwa kwaajili ya kuhojiwa ili kujua sababu za yeye kutotelekeza kazi hiyo
pamoja na mchakato wa kumlipa fedha zote hizo wakati kazi hiyo haina
thamani ya kulipwa fedha hizo.
Kwaupande wake mkuu wa Takukuru mkoa wa Rukwa
Hamza Mwenda aliahidi kutekeleza agizo hilo ili kuwaondolea kero wananchi wa
mji wa Matai ambao wamekuwa wakilalamikia kipande hicho cha barabara kwakuwa
kimekuwa kero kwakua ndicho kinacho chepuka na kuingia makao makuu ya wilaya
hiyo kutoka katika barabara kuu ya kutoka Sumbawanga mjini kwenda katika
bandari ya Kasanga.
Kweli inachosha sana, matai ni Mji ulio na wakazi wengi, pia wageni wanao ingia na kutoka ni wengi. Barbara hiyo itaongeza chachu kwa wananchi na wageni wanao ingia na kutoka.
ReplyDelete