Milion 30 Zatolewa Na Mmlaka Ya Bandari Tanzania Kusaidia Ujenzi.





Na Baraka  Lusajo- Rukwa.


MAMLAKA ya bandari Tanzania imekabidhi vifaa vya ujenzi kwa Zahanati
katika vijiji vya Kipili na Kabwe vyenye thamani ya Tshs,Mil.30 na
kusaidia ujenzi wa majengo ya Mama na mtoto katika mwambaao wa ziwa Tanganyika  mkoani Rukwa.

Akikabidhi vifaa hivyo kwa nyakati tofauti jana mwenyekiti wa bodi ya
Bandari Tanzania Prof,Ignas Rubaratuka alisema kuwa vijiji vya Kipili
na Kabwe vipo karibu na bandari hivyo katika kuweka mahusiano mema
wameonelea kusaidia katika sekta ya afya katika maeneo hayo ili
kupunguza changamnoto zinazoikabili sekta ya afya na kusaidia  wananchi  kutoka  wilaya  ya  kalambo na Nakasi wanaishi katika  mwambao wa  ziwa Tanganyika.

Alisema kuwa Zahanati hizo zipo mbali na hospitali ya wilaya hivyo ipo
sababu kwa Zahanati hizo kuwa na mazingira mazuri ya kihuduma ili
jamii inayopata huduma katika Zahanati hizo ipate huduma
zinazostahili na kwa muda muafaka.

Mbunge wa jimbo la Nkasi Kasikazini Ally Kessy kwa upande wake
alimshukuru Mwenyekiti wa bodi ya bandari Nchini kwa kutambua umuhimu
wa afya katika maeneo hayo na kuweza kutoa msaada huo na kuwa
atalisimamia jengo la Kabwe kuona linakamilika kwa wakati ila jeno la
kule Kipili limekamilika.

Alidai kuwa yeye kama mbunge ameendelea kuishukuru mamlaka ya bandari
kwa kuweza kfanikisha ujenzi wa bandari ya Kabwe jambo ambalo
amelipigania kwa muda mrefu na kuwa kasi iliyopo ya ujenzi wa bandari
hiyo ni nzuri na kuwa kama ikikamilika italeta mchango mkubwa wa
maendeleo katika ukanda mzima wa ziwa Tanganyika.

Mkurugenzi mtendaji wa wilaya Nkasi Misana Kwangula alimuhaidi
mwenyekiti wa bodi ya bandari kuwa watahakikisha ujenzi wa jengo la
Mama na mtoto linakamika kwa haraka ili kuona vifaa vilivyotolewa na mamlaka hiyo
vinafanya kazi iliyokusudiwa.

Alisema kuwa maeneo hayo ya Kipili na Kabwe yapo pembezoni sana mwa
wilaya na kuwa maeneo hayo yanatakiwa kuwa na huduma nzuri kwani ni
mbali sana kwa watu wa maeneo hayo kwenda kupata huduma hizo katika
hospitali ya wilaya.

Alivitaja vifaa vilivyopokelewa kuwa ni Saruji mifuko 256,Mabati gauge
28 pc 150,Vifuniko vya mabati 28 gauge Pc 5,Mbao 2x6x12 Pc 25,Mbao
2x4x12 Pc 60 na Mbao 1x10x12 Pc 15
Vingine ni Misumari ya bati Kg 10,Misumari mchanganyiko kg 11 na
Misumari Inchi 3kg 5 ambavyo vyote vimekabidhiwa katika zahanati hizo.

Akitoa shukrani kwa niaba ya Wananchi hao Diwani wa kata ya Kabwe
Ahsante Lubisha aliishukuru Mamlaka hiyo ya bandari kwa kujali afya ya
wakazi wa maeneo hayo ya Mwambao mwa ziwa Tanganyika na wao watatoa
ushirikiano wa kutosha katika kuona kuwa bandari ya Kabwe inakua
salama na kutoa mchgango mkubwa wa kiuchumi kwa taifa.



Comments