Horacio
Corbacho na Nicola Corradi, pamoja na muhudumu wa bustani, walipatikana na
hatia ya kuwabaka na unyanyasaji katika shule ya kikatoliki iliyopo katika
jimbo la Mendoza kuanzia mwaka 2004 hadi 2016.
Waathiriwa
kadhaa walikuwa mahakamani kushuhudia kutolewa kwa hukumu Jumatatu.
Kesi
hiyo imeishitua Argentina, nchi ambayo anatoka Papa Francis, huku wengi wakilishutumu
kanisa kwa kuzorota kuchukua hatua.
Kanisa
Katoliki limekabiliwa na shutuma za unyanyasaji wa kingono wa watoto katka
maeneo mbali bali duniani katka kipindi cha miongo michache iliyopita.
Mahakama ilibaini nini?
Jumatatu,
mahakama katika mji wa Mendoza alimhukumu kasisi wa Kiargentina kifungo cha
miaka 45 jela.
Padre huyo mwenye
umri wa miaka 59 alipatikana na hatia ya kuwanyanyasa kingono watoto katika
shule inayofahamika kama Instituto Antonio Provolo de Mendoza katika mji wa
Luján de Cuyo.
Corradi,
mwenye umri wa miaka 83-mwenye uraia wa Italia, alihukumiwa kifungo cha miaka
42 jela.
Alikuwa
anachunguzwa kwa unyanyasaji alioutekeleza katika shule ya Verona, nchini
italia miaka ya 1970, lakini hakuwahi kushitakiwa.
Armando
Gómez, muhudumu wa bustani katika shule ya Luján de Cuyo alihukumiwa kifungo
cha miaka 18 jela.
Hawawezi
kukata rufaa juu ya uamuzi wa mahakama kwa mujibu wa sheria za Argentina kuhusu
makosa hayo.
Comments
Post a Comment