Katikati ni mkuu wa wilaya ya Kalambo Julieth Binyura akikagua bidhaa mbalimbali. |
Mkuu
wa mkoa wa Rukwa Joachim Wangabo amewaagiza Wakurugenzi wa Halmashauri zote za
mkoa huo kusimamia kwa karibu uingizwaji wa pembejeo za kilimo na kuhakikisha
zinauzwa kwa bei elekezi ili kuwafikia wakulima kwa muda muafaka.
Akiongea
kupitia madhimisho ya ufunguzi wa msimu mpya wa kilimo kwa mwaka 2019/2020 Wilayani Kalambo,Mkuu wa Mkoa wa Rukwa
aliyewakilishwa na Mkuu wa Wilaya ya Kalambo
Julieth Binyura,amesema katika kipindi cha mwaka 2019/2020 mkoa unalenga kulima
jumla ya hekta 603,637.5 za mazao
mbalimbali.
‘’kati
ya hizo hekta 524,800.7 ni za mazao ya
chakula ,hekita 76,363.08 za mazao ya biashara na hekta 2,473.35 za
mazao mbalimbali ya mbogamboga na matunda. ‘’alisema Binyura .
Alisema
jumla ya tani 1,731,495.5 za mazao zinategemewa
kuzalishwa ambapo kati ya
kiasi hicho tani 1,602,5201.1 ni
za mazao ya chakula ,tani 115,800 za
mazao ya mbogamboga na matunda.
‘’nitoe maelekezo
kwa watendaji wote wa Halmashauri zote kuhakikisha mbolea hizi
zinauzwa kwa bei elekezi na zinawafikia wakulima katika maeneo yote’’alisema Binyura.
Mwakilishi
wa tasisi isiyokuwa ya kiserikali ya Briten, Progers Mbugi,amesema mpaka sasa
wameweza kufikia wakulima 54,000 kwa kuwapatia elimu na misaada mbalimbali.
‘’mpaka
sasa kupitia mradi huu tumeweza kuwafikia zaidi ya wakulima wadogo wadogo
54,000 wake kwa waume ,kutoka katika vyama vya msingi vya ushirika vya mazao –AMCOS pamoja
na wale walio nje ya vyama hivi. Lengo letu hadi kufikia mwisho wa mradi huu 2020 tuwe tume wafikia
wakulima 72,000.’’Alisema Progers Mbugi.
Kwa
upande wa wakulima wilayani humo wameiomba serikali kutoa pembejeo za kilimo mapema kabla ya msimu kuanza.
Comments
Post a Comment