Watu kadhaa wanahofiwa kufariki huko Tanganyika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo baada ya treni kupoteza muelekeo
Watu kadhaa wanahofiwa kufariki katika jimbo la Tanganyika huko Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo baada ya treni kupoteza muelekeo.
Waziri wa masuala ya kibinaadamu, Steve Mbikai ameithibitishia BBC kuwa watu 50 wanahofiwa kufariki katika ajali hiyo.
Mbikai ameelezea ajali hiyo kuwa janga jingine na kufahamisha kuwa mutano unaendelea kuratibu usaidizi wa dharura.
hHtahivyo gavana wa jimbo hilo amehoji idadi hiyo ya waziri ya watu waliofariki na kusema kwamba ni watu 10 waliofariki huku wengine takrian 30 wakiwa wamejeruhiwa
Duru kutoka shirika la kijamis ameiambia BBC kwamba treni hiyo ilikuw
ani ya mizigo iliyokuwa inasafriki kuelekea mji wa Kalemie.
Mapema Machi, watu kadhaa waliuawa katika ajali nyingine ya treni iliyopoteza muelekeo katika jimbo la kati la Kasai nchini Congo.
Ajali za reli hutokea nchini humo kutokana na miundo mbinu ya kitambo na isiyosimamiza kisawasawa.
Comments
Post a Comment