Wananchi Waiomba Serikali Kuongeza Vituo Vya Kupigia Kura.’’Kalambo’’

katika  picha  ni  msimamizi  wa  uchaguzi  wilayani  kalambo akiongea na wanahabari ofisini  kwake.


 Na Baraka Lusajo. Kalambo.

Zikiwa zimesalia siku chache kuanza kwa uchaguzi mkuu wa serikali za mitaa hapa nchini ,wananchi wilayani Kalambo mkoani Rukwa wameiomba serikali kuthibiti mianya ya  wahamiaji haramu kuingia nchini kinyemera sambamba na kuongeza vituo vya kupigia kura  pamoja na kuweka utaratibu maalmu kwa wazee na watu wasio jiweza ili kuwawezesha kushiriki kikamilifu katika zoezi hilo.

Jumla ya wananchi lakimoja kumi na nne elfu mia tisa hamsini na moja (114,951) wanategemea kuanza kupiga kura za kuwachagua viongozi wa serikali za vitongoji na vijiji ifikapo November 24,2019, ambapo kwa wilaya ya Kalambo zoezi hilo litafanyaka kwenye vijiji  mia moja kumi na moja(111) katika vituo mia nne ishirini na mbili(422).

Kufuatia umuhimu wa zoezi hilo wananchi wilayani humo wametoa maoni yao na huku wengi wao wakiomba serikali kuweka utaratibu mzuri ambao utasaidia akina mama wajawazito, wazee pamoja na watu wenye hali ya ulemavu kuweza kupiga kura kwa urahisi zaidi na kuchagua  kiongozi wanae mtaka.
‘’tunaomba serikali kuongeza vituo vya kupigia kura pamoja na kuweka utaratibu maalumu ambao utasaidia wazee pamoja na watu wenye hali ya ulemavu kupata huduma kwa urahisi zaidi kwa kuawachagua viongozi wanaotaka bila bugudha’’walisema wananchi hao.

Msimamizi mkuu wa uchaguzi wlayani humo Eriki Kayombo,amesema vituo vya kupigia kura vitafunguliwa kuanzia majira ya saambili asubuhi hadi saa kumi na moja jioni na kuwasihi  wananchi kujitokeza kwa wingi kuchagua viongozi wanao wataka kwa masirahi mapana ya  taifa.

‘’kura ni haki yako,kumbuka kupiga kura tarehe 24 november 2019 ili upate kiongozi bora atakae kuletea maendeleo na vituo vya uandikishaji vitafunguliwa kuanzia 2:00 asubuhi na kufungwa saa 12:00 jioni na vituo vya kupigia kura vitafunguliwa kuanzia saa2:00 asubuhi na kufungwa saa 10:00 jioni.’’alisema Kayombo.

Afisa uchaguzi wilayani humo Atanas Saida,amesema wamegawa vitendea kazi mbalimbali kwa  wananchi, mashirika ya dini pamoja na watu wengine.

‘’kusema kweli tumejipanga vizuri na mpaka sasa tumekwisha kugawa vifaa mbalimbali kwa mashirika ya dini watu maalufu, pamoja  na watumishi’’.alisema Saida.

Hata hivyo serikali wilayani humo imetangaza nafasi mianne ishirini na mbili za kazi ya  uandikishaji na uandaaji wa orodha ya wapiga kura ,zoezi ambalo litamudu  kwa muda  wa  siku saba.

Comments