kaptika picha ni mkuu wa wilaya ya Kalambo Julieth Binyura |
Na Baraka lusajo. Kalambo.
Ikiwa imesalia siku
moja kwa wanafunzi wa darasa la saba kuanza kufanya mtihani wa kuhitimu elimu
ya msingi hapa nchini,mkuu wa wilaya ya Kalambo Julieth Binyura amesema
hatasita kuwachukulia hatua kali za kisheria ikiwemo kuwafikisha mahakamani
wasimamizi wa mitihani ambao watakiuka maadili ya kazi yao na kufanya vitendo
vya undanganyifu wakati wa uendeshaji wa zoezi hilo.
Akiongea ofisini
kwake mkuu wa wilaya hiyo Julieth Binyura kupitia mahojiano maalumu na kituo hiki,
amesema Jumla ya wanafunzi 3765 wanategemea kuanza kufanya mtihani wao wa kuhitimu
elimu ya msingi kuanzia sptember 11,2019 na huku kati yao hao wavulana ikiwa ni
1854na wasichana 1872.
Aidha amewataka
wananchi kuendelea kuwaombea kwa mungu wanafunzi wote ili waweze kufanya vizuri mitihani yao na kufaulu vizuri na hatimaye
kujiunga na elimu ya sekondari.
Badhi ya
wanafunzi wilayani humo wamesema wamejiandaa
vuziri na wanaimani watafanya vizuri mitihani hiyo.
Mitihani ya kuhitimu elimu
ya msingi inategemewa kuanza
sptember 11,2019 na kumalizika sptember 12, 2019 katika shule za msingi
97 za wilaya hiyo.
Comments
Post a Comment