katika picha ni mkuu wa wilaya ya Kalambo Julieth Binyura |
Na Baraka Lusajo.Kalambo.
Mkuu
wa wilaya ya kalambo Julieth Binyura amemwagiza mkurugenzi mtendaji wa
halmashauri hiyo Msongela Palela kufuatilia na kuwachukulia hatua kali za
kinidhamu wahudumu wa afya ambao wamekuwa wakitoroka muda wa kazi kwenye vituo
vyao na kupelekea malalamiko kutoka kwa wagonjwa kutokana na kukosa huduma kwa
muda unaostahili.
Ameyasema
hayo wakati akisikiliza kero mbalimbali za wananchi kupitia mkutano wa hadhara
uliojumuisha vijiji nane kutoka kata za Lyowa na Matai wilayani kalambo mkoani
hapa na kuwasisitiza wahudumu wa afya kufanya kazi kwa bidii na kuondokana na vitendo vya
utoro kwenye maeoneo yao ya kazi kwa lengo la
kuondokana na malalamiko yasiyo kuwa ya lazima kutoka kwa wananchi.
‘‘Hili
nalikemea lisitokee tena na sasa naanzisha utaratibu wa kukagua nyakati za
usiku na ambaye nitakuta hayupo nitamchukulia hatua kwani atakuwa amevunja sheria.’’ Alisema Binyura.
katika picha ni kaimu mkurugenzi Efraim Moses |
Kaimu
mkurugenzi wa halmashauri hiyo Efraim Moses Mwalemba amewataka madiwani kushirikiana na watendaji wa kata na
vijiji katika kukusanya mapato ambayo yatasaidia kuendeleza shughuli za
maendeleo.
‘’Waheshimiwa
madiwani ndio wenye jukumu la kukusanya mapato wakishirikiana na watendaji
wa vijiji na kata kwenye maeneo yao husika kwani fedha hizi huwa zinatumika
katika shughuli mbalimbali za
serikali ikiwemo kuendeleza miradi ya
Serikali, kulipa posho za madiwani na mambo mengine yahusuyo usitawi wa
Halmashauri.’’alisema Moses
Comments
Post a Comment