Wadau Watakiwa Kutoa Elimu Kwa Wananchi Juu Ya Umuhimu Wa Kupiga Kura.

katika picha ni baadhi  ya  watumishi wamipewa  elimu  juu  ya umuhimu  wa zoez  laa upigaji kura

Haki,usawa na wajibu vimetajwa kuwa nyenzo muhimu katika makuzi na mwendelezo wa amani kwa maendeleo ya Wilaya ya Kalambo, Tanzania na bara la Afrika kwa ujumla.

Akiongea katika kikao cha wadau wa uchaguzi kilicho wajumuisha viongozi, mila Taasisi na watu maarufu Wilayani Kalambo,Msimamizi wa uchaguzi Wilaya ya Kalambo Erick John Kayombo, amesema wadau hao wana wajibu wa kushirikiana na Serikali kuelimisha Wananchi juu ya umuhimu wa kushiriki uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaotarajiwa kufanyika Kitaifa Tarehe  24/11/2019 kwa ari na mshikamano kwa kuzingatia haki na usawa ili kuendeleza amani na umoja wa Kitaifa.

Wilaya ya Kalambo inayokadiliwa kuwa na jumla ya watu 271,393 wakiwemo wanaume 131,285 na wanawake 140,108 ambao wote wanatakiwa kuhamasishwa vilivyo ili washiriki uchaguzi wa Serikali za mitaa tarehe 24/11/.2019,Ina jumla ya vitongoji 422,Vijiji 111 kata 23 na tarafa 4.ikiwemo Matai,Kasanga,Mwimbi na tarafa ya Mambwe inayopakana na nchi jirani ya Zambia kwa upande wa Kasikazini pamoja na Wilaya ya Momba upande wa kusini Mashariki.

Msimamizi wa uchaguzi Wilaya ya Kalambo Erick John Kayombo, amesisitiza kuwa maendeleo hayawezi kuja kama Jamii haitakuwa na uongozi bora,

“Nadharia za kale za wanafalsafa kama vile Cara Max na John Luke zinamwelezea mwanadamu kuwa ni mnyama wa kisiasa anayehitaji kuongoza na kuongozwa ili pawepo na amani na kujihakikishia maendeleo ya kweli katika jamii.

‘’ tukiwa wadau wa uchaguzi Wilayani Kalambo tunawajibu wa kuihamasisha jamii kujitokeza kuandikishwa kwenye daftari la wapiga kura na kuchukua fomu za kugombea nyadhifa mbali mbali kam vile uenyekiti wa vijiji na vitongoji pamoja na ujumbe wa Serikali za vijiji ifikapo tarehe 29/10/2019.’’ Anafafanua Erick Kayombo.

Comments