Wachungaji Walalamikiwa Kufungisha Ndoa Waumini Bila Kuwapima Ukimwi.







katika picha ni mkurugenzi  wa SUCODA


Na Baraka Lusajo. Kalambo.
Wadau kutoka asasi zisizo kuwa za kiserikali zinazohusika na maswala ya ukatili wa kijinsia mkoani Rukwa wamelalamikia kitendo cha baadhi ya wachungaji na watumishi  wengine  wa mungu kuto pima afya za waumini wao pindi wanapofunga ndoa na hivyo kupelekea kujitokeza migongano ya kifamilia kutokana na baadhi yao kukutwa na mambukizi ya virusi vya ukimwi.
Katika picha ni washiriki wa mafunzo ya  ukatili wa kijinsia.
Kumekwepo na mamalamiko kutoka kwa wananchi mkoani Rukwa juu ya kujitokeza kwa migogoro ya kifamilia ambayo imekuwa ikisababishwa na baadhi ya wachungaji na watumishi wengine wa mungu kudaiwa kuto wapima wanandoa hao kabla ya kufungishwa ndoa .

Hali hiyo imepelekea wadau wanaohusika na maswala ya ukatili wa kijinsia na mila potofu kutoka Asasi ya Sumbawanga Community Development Achievement (SUCODA) kuingilia kati swala hilo kwa kutoa elimu  kwa wachungaji,mashehe, watumishi wa serikali pamoja na watu wengine, lengo likiwa ni kutoa elimu juu ya umuhimu wa watu kupima kabla kufunga ndoa.

’tumeona ni vyema tukakaa na wachungaji ili kuwapatia mafunzo zaidi juu ya maswala ya ukatili  wa kijinsia kwani kitendo cha mchungaji kufungisha ndoa bila kujua afya za wahusika, ni kitendo kibaya kwani kina sababisha kuongezeka kwa magonjwa ya ukimwi.’’alisema Mwazyunga.

Afisa maendeleo ya jamii wilayani humo Yasinta Nkyabonaki,amesema hali hiyo imekuwa ikisabisha kuongezeka kwa mambukizi ya virusi vya ukimwi pamoja na migogoro ya kifamilia.
Katika picha ni afisa ustawi wa jamii wilayani kalambo
Alphonsa Shirima afisa ustawi wa jamii wilayani humo,amesema wazazi wanawajibu wa kuwal

ea watoto  wao katika mazingira bora ikiwemo kuwapatia mahitaji yote muhimu.
katika picha ni mwanasheria  kutoka shirika  la Sucoda.
 Kwa upande wake mwanasheria kutoka Asas isiyokuwa ya kiserikali ya SUCODA Jonas

Chidowi, amesema ni kosa kisheria kwa wachungaji kuto pima afya za watu wanao funga ndoa.

‘’niwasihi wachungaji kujenga mazoea ya kupima afya za waumini wao hususani wale ambao wanaokuwa  kwenye harakati za kuoa ama kuolewa kwa lengo la kupunguza kasi ya mambukizi ya ukimwi.alisema Chidowi.

Kwa upande wake mchungaji kutoka kanisa la Moravian katika wilaya ya Kalambo Tedysoni Nzalamwe, amesema changamoto  kubwa  imekuwa  ikijitokeza  kutokana na taarifa feki  kutoka kwa wanandoa  wenyewe ambazo zimekuwa  zikisababisha wao kuingia  kwenye migogoro.

0746248872.


Comments