TALGWU WATAKA HAKI ZA WAFANYAKAZI KUPEWA KIPAUMBELE.


Na mwandishi  wetu.Sumbawanga.

Mkutano mkuu wa chama cha wafanyakazi wa serikali za mitaa-TALGWU- mkoa wa Rukwa umewaagiza makatibu wa halmashauri zote nne za mkoa huo kutumia msaada wa kisheria ili kuwathibiti badhi ya waajiri wanaotuhumiwa kudhulumu  haki na stahili za wafanyakazi wao.

katibu wa TALGWU mkoa wa Rukwa, Sospeter Challo amezitaja baadhi ya haki na stahili wanazodhulumiwa  wafanyakazi katika halmashauri za wilaya ya Sumbawanga, Nkasi, Kalambo na manispaa kuwa ni pamoja na kunyimwa masurufu ya uhamisho na kuelezea moja ya maazimio ya mkutano mkuu wa chama hicho katika kuthibiti haki za watumishi wanapopata uhamisho haki zinazodaiwa kuminywa na baadhi ya waajiri.

Mgeni rasmi katika mkutano huo wa TALGWU ngazi ya mkoa mkuu wa wilaya ya Sumbawanga dokta Halfany Haule ,amesema baadhi ya watumishi katika serikali za mitaa wanatuhumiwa kushindwa kutimiza wajibu wao kwa ajili ya kutaka kujinufaisha  wenywewe.

mkutano mkuu wa siku mbili wa wajumbe wa mkutano mkuu wa chama cha wafanyakazi wa serikali za mitaa-TALGWU-mkoa wa Rukwa umehusisha pia mafunzo ya uelewa wa sheria mahali pa kazi

Comments