Mkuu wa mkoa wa Rukwa Mh.Joachim Wangabo amewataka wakala wa
taifa wa hifadhi ya chakula (NFRA) Sumbawanga kuharakisha ujenzi wa vihenge
unaogharimu kiasi cha shilingi bilion 15 kwa kushirikiana na wakala wa majengo Tanzania kwa lengo la kusaidia
wakandasi kuto fanya makosa wakati wa zoezi hilo.
Amesema kuwa ujenzi huo wa vihenge ni mkubwa na unagemewa kutoa
ajira mbalimbali na hivyo kuwataka wananchi wa mji wa sumbawanga na maeneo
mengi ya Mkoa kutoa kuchangamkia fursa ya ajira katika ujenzi
utakaogharimu karibu shilingi bilioni 15 na hivyo kuwataka Wakala wa Taifa wa
hifadhi ya Chakula (NFRA)Sumbawanga kuhakikisha wanasimamia vizuri kwa msaada
na ushauri kutoka Wakala wa Majengo Tanzania wakihakikisha mkandarasi hafanyi
makosa.
“Tulichelewa kuanza huu ujenzi lakini tulitaka huu ujenzi wa
vihenge uje katika eneo hili la viwanda la Kanondo, Hii kazi naona mmeanza
vizuri pamoja na kuchelewa tangu mwezi wa saba, tunategemea mwezi wa saba
mwakani hivi vihenge sita viwe vimekamilika pamoja na ghala lake moja na uwezo
wa vihenge pamoja na ghala ni kuhifadhi tani 26,000 na vikikamilika NFRA
watakuwa na uwezo wa kuhifadhi tani 59,500 hii ni mara mbili ya uwezo tulionao
sasa hivi, hivyo tunawahamasisha wakulima walime mahindi kwa wingi, uhakika wa
soko upo,” Alisisitiza.
Wakati akitoa taarifa ya ujenzi huo Meneja wa NFRA kanda ya
Sumbwanga Abdillah Nyangasa alisema kuwa NFRA wana maghala katika maeneo matatu
ndani ya mkoa wa Rukwa moja likiwa Halmasharu ya Wilaya ya Sumbawanga katika
mji mdogo wa Laela na mawili yakiwa katika Manispaa ya Sumbawanga katika eneo
la Mazwi pamoja na eneo la Kanondo.
“Kwa upande wa Mazwi tuna maghala yenye uwezo wa kuhifadhi tani
18,500 ambapo hali yake mengi ni machakavu yanahitaji ukarabati pia mazwi hapo
hapo tuna ghala la tani 4000 ambalo nalo ni chakavu na lilitakiwa kufanyiwa
ukarabati kama mradi huu ungefanyika pale lakini hapo mazwi kuna maghala mawili
ya tani 3000 na kufanya tani 6000 ambayo hayo hayahitaji ukarabati na
ndipotulimohifadhia mahindi, lakini kuna ghala la Laela ambalo lina uwezo wa
kuhafadhi tani 5000 hili linahitaji ukarabati kidogo kwa ndani, lakini pia kuna
mradi huu mpya wa kanondo,” Alisema.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa manispaa ya Sumbawanga Jacob
Mtalitinya alisema kuwa Eneo hilo la Viwanda na maghala lina viwanja 103 na
viwanja 43 tayari vimeshauzwa na kuongeza kuwa ujio wa ujenzi wa vihenge hivyo
utasaidia kuongeza thamani ya eneo hilo kwasababu ilikuwa inaonekana
miundombinu bado haijafika lakini kutokana na ujenzi wa vihenge hivyo
halmashauri imefanikisha kufikisha umeme na maji katika eneo hilo na kuongeza
kuwa Manispaa inamradi mkubwa wa maji unaotarajiwa kusambaza maji katika eneo
hilo.
“Tunawaomba wananchi wa Sumbawanga na wawekezaji kutoka nje kuja
kuwekeza kwani sasa eneo letu lipo hai na limeanza kufanyiwa kazi, waje
wawekeze viwanda mbalimbali, hata wafanyabiashara wetu wa pale mjini lakini
mheshimiwa mkuu wa mkoa kwa kuongeza tunategemea nasi Manispaa kuchukua viwanja
viwili ambapo tutajenga sehemu kwaajili ya wafanyabiashara wadogowadogo walipo
pale mjini waweze kuhamia hapa,” Alimalizia.
Ujenzi huo wa vihenge vipya vya kisasa unaojengwa na
mkandarasi Elerai Construction Company Limited kwa ufadhili wa Serikali ya
Poland wenye thamani ya Shilingi bilioni 13.6 unatarajiwa kumalizika mwezi
July, 2020 na kuongeza uwezo wa kuhifadhi chakula kutoka tani 33,500 za sasa
hadi kufikia tani 59,500 na hivyo kuongeza ununuzi wa zao la mahindi wa NFRA
kutoka kwa wakulima.
Comments
Post a Comment