Prince Harry atembea katika ardhi ya mabomu yaliyofukiwa ardhini Angola

Prince Harry walking through a minefield in AngolaKatika sehemu ya ziara yake kusini mwa Afrika, Mwana mfalme Harry ametembelea nchini Angola ili kuendeleza jitihada za kuondoa mabomu yaliyo ardhini.
Mwana mfalme huyo ameamua kufuata nyayo za mama yake, Princess Diana ambaye mwaka 1997 alitembelea maeneo hayohayo na kutaka kuondoa mabomu yaliochimbwa ardhini.
Picha za ziara yake zilipendwa na wengi duniani kote.
Eneo hilo hatari bado linaendelea kumaliza maisha ya watu wengi katika nchi nyingi.
Je, sehemu hizo ziko katika maeneo gani duniani na hatua gani zimechukuliwa?

Jinsi Prince Harry anavyofuata nyayo za mama yake

Princess Diana walking through a landmine field in Angola in 1997Haki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Princess Diana alijulikana sana kwa kujitolea kwa wahitaji ingawa mafanikio yake hakuyaweka hadharani.
Kwa mfano Diana alifungua kliniki ya kwanza Uingereza kwa ajili ya waathirika wa virusi vya ukimwi mwaka 1987, na kuweza kufanikiwa kubadili tabia za waathirika
Kuhamasisha uwelewa juu ya mabomu yaliyochimbwa ardhini, ni miongoni mwa kosa kubwa lililosababisha apewe talaka na mume wake Prince Wales mwaka 1996.
Kwa miongo kadhaa mabomu ya ardhini yalikuwa yamaetumika katika migogoro mingi.
Mabomu mengi ambayo hayajalipuka yaliachwa wakati wa vita, kipindi ambacho mauaji ya watu yalifanyika kwa wingi au yalilipuka bila kutarajiwa.
Princess Diana with children in AngolaHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Picha inaonyesha namna wakazi wa Angola walivyoathirika na vilipuzi hivyo.
Wakati wa ziara yake Prince Harry ameelezea mabomu hayo yaliyochimbiwa ardhini ni kovu la vita lisilopona .
Vilipuzo hivyo vimesababisha mauaji ya watu wa ngapi na wangapi wameumia?
Radio controlled mine clearance machine in AngolaHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Mabomu hayo ambayo yaliyofukiwa ardhini huwa yanalipuka kwa makubaliano fulani au bila kulipuka bila kutarajiwa.
Kuna aina mbili ya mabomu: Mabomu yaliyofukiwa yakiwa yanalenga kujeruhi watu au kuwauwa na aina ya pili ya mabomu yametengenezwa kwa ajili ya kuteketeza magari.
Vilipuzi hivyo vilitumika katika vita ya kwanza ya dunia, lakini yalianza kulipuka kuanzia mwaka 1960 na kuendelea.

Comments