Madiwani Wilayani Kalambo Wapiga Marufuku Magari Ya Mizigo Kusafirisha Mazao Nyakati Za Usiku


Na  Baraka  lusajo. Kalambo.

katika picha ni madiwani wilayani kalambo
Mkutano wa baraza la madiwani katika halmashauri ya wilaya ya kalambo mkoani Rukwa umewapiga marufuku wafanyabishara wote kusafirisha mizigo ya mazao nyakati za usiku ikiwa ni jitihada za kudhibiti upotevu wa fedha za mapato na kumtaka mkurugenzi mtendaji wa halmashauri hiyo Msongera paela, kuhakikisha anaweka migambo kwenye mageti yote sambamba na kuweka utaratibu mzuri wa kukusanya  fedha  kutoka kwa watendaji wa vijiji.

Halmashauri ya wilaya ya kalambo katika kipindi cha mwaka wa fedha 2018/2019 ilikuwa na makisio  ya  kukusanya  fedha kupitia  vyanzo vyake vya  ndani kiasi cha shilingi bilion mbili na kufanikiwa  kukusanya kiasi  cha shilingi bilioni moja  nukuta mbili sawa na asilimia 61.05.

Awali wakiongea kupitia kikao cha baraza la madiwani wilayani humo, wamesema kwa  mwaka  2019 na 2020 wameazimia  kufikia  malengo ya ukusanyaji mapato kwa  kushirikina na watendaji  wa vijiji na kata na kumshauri mkurugenzi mtendaji kutowaruhusu watendaji kukaa na fedha za makusanyo kwa muda mrefu.
mkurugezi mtendaji  wilayani kalambo

Mkurugezi mtendaji wa halmashauri hiyo   Msongera palela ,amesema  wamejipanga  kubuni vyanzo vipya vya mapato nakuwasihi madiwani kutoa ushirikiano katika zoezi zima la ukusanyaji mapato.

‘’Tumejidhatiti kuanzisha zoezi la kutoa hati za ardhi za kimila na leseni za makazi kwa wananchi pamoja na kutoa elimu juu ya manufaa ya mpango huo ili Halmashauri ipige hatua mbele’’alisema msongela.

Katibu tawala wilayani humo Frank Sichalwe, amesema ofisi ya mkuu wa wilaya itaendelea kuwasaka na kuwachukulia hatua watendaji wote ambao washindwa  kufanya marejesho ya fedha za mapato  kwa muda muafaka.
’ofisi ya mkuu wa wilaya kwa kushirikiana na ofisi ya mkurugezni mtendaji wa halmashauri itaendelea kuwasaka na kuwachukulia  hatua waatendaji ambao  wagundulika kukaa na fedha majumbani kama ilivyo  fanya kwa  mwaka wa fedha uliopita’’ alisema sichalwe.

Comments