Na Baraka Lusajo. Kalambo
Halmashauri ya wilaya ya kalambo mkoani Rukwa kupitia idara ya mifugo na uvuvi imenza kukabiliana na wimbi la mbwa vichaa kwa kuwapiga risasi baada ya kujitokeza
malalamiko ya wananchi katika maeneo tofauti ya wilaya hiyo wakidai kung’atwa
na kusababishiwa madhara mbali mbali yakiwemo tetenasi, kichaa cha mbwa na
hatimaye kupoteza maisha.
Hatua hiyo inakuja baada ya mbwa mmoja aliyesadikiwa kuwa na
kichaa kung’ata watoto kumi na nne katika vijiji vya Keleni na Matai asilia,
watu wazima watatu Kisungamile na mtu mzima mmoja katika kijiji cha Santa Maria
ambaye pia alipoteza maisha. Kufuatia matukio hayo, wananchi wamelazimika kuiomba
serikali kuangalia namna ya kuwasaidia kwa kuawapatia chanjo mbwa wote.
‘’Tunaiomba serikali
iangalie uwezekano wa kuwa chanja mbwa wote pamoja na kusogeza huduma ya chanjo
ya kuzuia kichaa cha mbwa kwenye Vituo vya Afya na Zahanati zote, badala ya
kufuata huduma hiyo mjini Sumbawanga baada ya kung’atwa na mbwa ambapo baadhi
ya watu wamekuwa wakichelewa na hatimaye kupoteza maisha.’’Walisema
wananchi hao.
Akiongea kupitia mkutano wa hadhara uliofanyika katika Kijiji
cha Santa Maria, Afisa mifugo na uvuvi wilayani humo Wilbroad Kansapa, amesema
wilaya hiyo inajumla ya
mbwa wapatao 6,360 na kwamba ili
kukabiliana na changamoto hiyo amewasiliana na Mganga Mkuu wa wilaya ili
kuhakikisha dawa za kuwatibu watu ambao wamekuwa wakiathirika na adha hiyo
zinapatikana kwenye vituo vyote vya afya
na zahanati katika Wilaya nzima.
Wakati huo huo ,amewataka wananchi wote wanaomiliki mbwa
kuwaleta mbwa wote kuchanjwa pindi tangazo linapotolewa, na kwamba mbwa wote
lazima wafungwe kuanzia saa kumi na moja asubuhi na kufunguliwa saa sita usiku,
vinginevyo hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yao wote watakao kaidi
sheria hiyo, lengo likiwa ni kuendeleza azima ya Serikali ya kufuga kitaalamu
na kwa tija nchini kote.
-
Comments
Post a Comment