Erick Kabendera: Mwandishi anayeshikiliwa Tanzania afanyiwa vipimo

KabenderaMwandishi wa habari za uchunguzi nchini Tanzania, Erick Kabendera, anayetuhumiwa kwa makosa ya uhujumu uchumi, ameieleza mahakama nchini humo kuwa ameanza kupelekwa hospitali.
Kabendera alionekana akiuvuta mguu wake, na kuwa kwenye maumivu wakati alipopandishwa kizimbani Septemba 12, na mawakili wake kuiambia mahakama kuwa mteja wao ana matatizo ya kupooza mguu wa kulia na pia kupumua kwa shida.
Hii leo kwa mujibu wa gazeti la Mwananchi, Kabendera amethibitisha kuwa jana Jumanne Septemba 17, 2019 alipelekwa Hospitali ya Rufaa ya Amana na amefanyiwa kipimo cha X Ray kwenye mgongo pamoja na kipimo cha damu.
"Nashukuru jana nilifanikiwa kwenda Hospitali ya Rufaa ya Amana na nilifanyiwa kipimo cha X Ray kwenye mgongo wangu na majibu yametoka," amedai Kabendera.
Kabendera amedai alikuchukuliwa kipimo cha damu na majibu yake bado hajapewa, na yanasubiriwa ilia aanze matibabu.
Pia ameieleza mahakama kuwa bado ana maumivu makali katika mguu wake.
Upande wa mashataka umedai kuwa bado haujakamilisha upelelezi na Hakimu Mkazi Mwandamizi wa Mahakama ya Kisutu Agustine Rwizile ameahirisha kesi hiyo hadi Oktoba 1, 2019.

Mashtaka dhidi ya Kabendera

Kabendera alipandishwa kizimbani Agosti 5 na kusomewa mashtaka matatu ya ubadhirifu wa kiuchumi .
Katika mashtaka hayo Kabendera anatuhumiwa na kujihusisha na genge la uhalifu na uhujumu wa uchumi nchini Tanzania, shtaka la pili ni la kukwepa kulipa kodi ya zaidi ya milioni mia moja sabini za kitanzania.
Kosa la tatu ni la utakatishaji fedha zenye thamani ya zaidi ya millioni mia moja na sabini.
Kwa mujibu wa mashtaka yaliowasilishwa, Kabendera anadaiwa kuyatekeleza hayo baina ya Januari 2015 na Julai mwaka huu mjini Dar Es Salaam na kwa baadhi ya makosa anadaiwa kuyafanya kwa ushirikiano wa watu ambao hawakuwepo mahakaman

Comments