Ded Kalambo Azitaka Kamati Za Ukatili Wa Kijinsia Kutoa Elimu Sahihi Kwa Wananchi.



Katika picha ni mkurugezi mtendaji kalambo.
Na Baraka Lusajo- Kalambo.

Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Kalambo Mkoani Rukwa Msongela Palela amezitaka kamati zote zinazohusika na maswala ya ukatili wa kijinsia kushirikiana na viongozi wa serikali za vijiji na kata katika kutokomeza mila potofu zilizojengeka katika jamii na kuwaagiza maafiasa maendeleo ya jamii kufuatilia na kutoa ripoti sahihi juu ya utekelezaji wa kazi hizo.

Ameyasema hayo wakati wa uzinduzi wa kamati za kupinga ukatili na mila potofu wilayani Kalambo mkoani hapa,ambapo amesema lengo la serikali ni kuhakikisha ukatili wa kijinsia na mila potofu zinatokomezwa katika jamii kwa kutoa elimu sitahiki kwa wananchi.

Amesema kamati hizo zitafanyakazi katika kata ishirini na tatu za wilaya hiyo na kuzitaka  kamati  hizo  kuhakikisha elimu waliopatiwa inawafikia wananchi wote kwa muda muafaka.

‘’yale malengo tuliojiwekea ndio tukayatekeleze na mtakapo  rudi katika  vijiji na kata  zenu nendeni mkawe walimu wazuri kwani hivi leo mmefundishwa ili mkawafundishe wengine’’.alisema Msongela.
katika picha ni mwezeshaji wa mafunzo, Faustina Valeli

Mwezeshaji wa mafunzo hayo Faustina Valeli amezitaka kamati hizo kufichua matukio ya ukatili wa kijinsia sambamba na kuwachukulia hatua kali wahusika wa matukio hayo kwa kuwafikisha kwenye vyombo vya dora kwa hatua zaidi za kisheria.
katika picha ni mkurugenzi  wa asasi  yaSucoda.

Mkurugezi kutoka Asasi isiyokuwa ya kiserikali ya Sukoda Samweli Mwazunga,amesema mradi huo  utajikita zaidi katika kutoa  elimu kwa jamii  juu na namna  ya kuepuka ukatili wa kujinsia na Mila potofu katika jamii.

Mafunzo hayo yameshirikisha walimu wa shule za msingi na sekondari, Wahudumu wa afya vijijini (WAVI) , maafisa maendeleo ya jamii pamoja na watendaji .

mawasiliano zaidi. 0762432747.

Comments