Na Baraka Lusajo. Kalambo
Zikiwa
zimesalia siku chache wanafunzi wa darasa la saba kuanza mitihani ya kuhitimu
elimu ya msingi,Mkuu wa wilaya ya kalambo Julieth Binyura amewaagiza maafisa elimu
wilayani humo kuwachukulia hatua kali za kisheria ikiwemo kuwafikisha mahakamani
wazazi na walezi ambao watagundulika kuwashawishi watoto wao kufanya mitihani
yao vibaya kwa lengo la kuwasaidia kazi
za nyumbani.
Julieth Binyura-mkuu wa wilaya ya Kalambo akiongea na wananchi katika mji wa Matai. |
Kumekuwepo
na changamoto ya baadhi ya wazazi na walezi wilayani humo kuwashawishi watoto
wao kufanya vibaya mitihani ya kuhitimu elimu ya msingi kwa lengo la kuwasaidia kufanya kazi za nyumbani
zikiwemo kilimo,kuchunga ng’ombe na watoto wa kike kuwaozesha.
Hali
hiyo imepelekea mkuu wa wilaya hiyo
Julith Binyura Kuingilia kati swala hilo kwa kuitisha mkutano wa hadhara
uliofanyika katika kata ya Matai na
kuwataka wananchi kutoa taarifa
za uwepo wa vitendo
hivyo ili wahusika waweze kukamatwa na kuchukuliwa hatua za kisheria.
Amesema
serikali
haita wafumbia macho wazazi
na walezi watakaokamatwa kwa tuhuma
za kuwaachisha masomo
watoto wao kwa
kuwapeleka mashambani au
machungani.
‘’kunatabia za baadhi ya wazazi
ambao wana waambia watoto mkaandike vibaya vibaya sasa tutakaye mgundua ataenda
jela akatumikie kifungo. Hivyo nimarufuku wazazi kuwaambia watoto mkaandike
vibaya.
Efraim Moses kaimu mkurugenzi -kalambo |
‘’Niwatake wanafunzi kutoa taarifa kwa walimu
kama wazazi wenu watawashawishi kufanya
mitihani vibaya. Niwatake pia wazazi muwaache wanafunzi wasome kwa amani
na tuna imani mwaka huu
wanafunzi wote watafaulu’’.alisema Binyura.
Kwa
upande wake kaimu Mkurugenzi wa halmashauri hiyo Efraim Moses Mwalemba, amesema
lengo la serikali ni kuhakikisha kila
mtoto anapata elimu sitahiki.
Amesema
wazazi
wanatakiwa kuwa na uelewa
sahihi juu ya umuhimu
wa elimu kwa
kuwapeleka watoto wao shule kama
Serikali ya awamu ya tano inavyotoa sera
ya elimu bure kwa wanafunzi wa shule za
msingi na Sekondari
Hata
hivyo kwa mwaka 2019 wanafunzi 3724 wilayani humo wanategemea kuanza mitihani
yao ya kuhitimu elimu ya msingi na huku
mitihani hiyo ikitegemewa kuanza kufanyika Sptember 11 hadi 12 ,2019.
Comments
Post a Comment