katika picha ni wafanyakazi wa kampuni ya kichina |
Na Baraka Lusajo.Kalambo.
Mkuu wa wilaya
ya Kalambo mkoani Rukwa Julieth Binyura ametoa siku saba kwa kampuni ya kichina
inayotengeneza barabara ya lami kutoka Sumbawanga-Matai-Kasanga mwambao wa ziwaTanganyika
kulipa mishahara pamoja na kutoa mikataba kwa wafanyakazi wao na kuahidi
kuwaweka ndani viongozi wote wa kampuni
hiyo endapo watashindwa kutekeleza agizo hilo.
katika picha ni mkuu waa wilaya ya Kalambo Julieth Binyura. |
Kumekwepo na malalamiko ya muda mrefu kutoka kwa wafanyakazi wa kampuni ya kichina ya‘’Joint Venture of China Railway 15G and new centry co ltd’’ kutotoa mikataba pamoja kutopeleka fedha kwenye mfuko hifadhi wa taifa wa jamii NSSF licha ya wafanyakazi hao kukatwa fedha na kamapuni hiyo kupitia mishara yao na kumtaka mkuu wa wilaya hiyo kuingilia kati swala hilo.
Awali
wakiongea mbele ya mkutano wa hadhara ulifanyika katika kata Kasanga wilayani humo
,wamesema wanahofu na mashaka juu ya kutolipwa sitahiki zao kutokana na mradi
huo kutakiwa kukamamilika November 2019 na kuwa kila wakienda NSSF kufuatilia
mafao yao wamekuwa wakiambiwa kuwa hakuna fedha zilizoingizwa kwenye acont zao na mwajiri wao.
Wamesema
serikali kupitia mkuu wa wilaya haina budi kuingilia kati swala hilo kwa kutoa
maagizo kwa wahusika ili waweze kuingiziwa fedha zao kwenye mfuko wa hifadhi ya
jamii.
Jacksoni
Mayunga mmoja wa wafanyakazi wa kampuni hiyo,amesema licha ya hilo
wafanyakazi waliowengi kwenye kampuni hiyo
hawana mikataba na wengine wamekuwa wakifukuzwa kazi bila kupewa
barua hali ambayo imekuwa ikiwapatia ugumu hususani wakati wa kudai
mafao yao NSSF.
Meneja wa NSSF
mkoani Rukwa Salawa Hangumbalo,amesema endapo fedha zikipelekwa NSSF wafanyakazi
wote watalipwa na kuwasihi wafanyakazi hao kufika kwenye ofisi za mfuko huo kutoa taarifa pindi
kunapotokea changamotoa yoyote.
katika picha ni meneja wa NSSF mkoani Rukwa |
mkuu wa wilaya
hiyo Julieth Binyura amelazimika Kuingilia kati swala hilo na kutoa siku saba kwa
kamampuni hiyo kupeleka fedha kwenye mfuko wa hifadhi ya jamii wa taifa NSSF pamoja na kutoa
barua za wafanyakazi wote ambao
walikuwa wameachishwa kazi kwa lengo la kuondokana na migogoro isiokuwa
ya lazima.
‘’natoa
maagizo kwa uongozi
wa kampuni hii ,nataka ndani ya siku
saba mtoe barua kwa wafanyakazi
wote ambao walikuwa wameachishwa
kazi pia mtoa mikataba kwa kila
mafanya kazi wenu na endapo mkishindwa kufanya hivyo mkurugezi wa kamapuni
pamoja na viongozi wengine nitawaweka nadani’’Alisema Binyura.
Mradi wa ujenzi wa
barabara ya lami ya Sumbawanga – Matai –
Kasanga yenye urefu wa km107 unafadhiliwa na Serikali ya Tanzania na kugharimu
Shilingi Bilioni 133.2 ambapo ujenzi wake unategemewa kumalizika mwezi November 2019 chini ya Mkandarasi Joint Venture of
China Railway 15G/New Century Company Ltd.
0762432747. maswaliano zaidi.
Comments
Post a Comment