Na Baraka Lusajo,Kalambo.
Chama
cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Kalambo Mkoani Rukwa kimewataka vijana kujenga
mazoea ya kushiriki kwenye michezo mbalimbali ambayo imekuwa ikianzishwa na
wadau kwa lengo la kuwasaidia kuimarisha afya zao na kujiajiri wenyewe.
Kumekuwepo
na changamoto ya baadhi ya vijana kushindwa kushiriki kwenye michezo ambayo
imekuwa ikianzishwa na wadau mbalimbali kutoka ndani na nje ya mkoa na hivyo
kupelekea Chama cha Mapinduzi wilayani humo kuchukua hatua ya kuanzisha
ligi ambayo itashirikisha zaidi ya timu sita katika Tarafa
ya Mwazye wilayani humo.
Akizindua
michezo hiyo Katibu wa itikadi, siasa na uenezi wilayani humo John Mbita, amesema
lengo la michezo hiyo ni kuhakikisha vijana wanashiriki kikamilifu kwenye
michezo
‘’Chama
cha Mapinduzi kata ya Mwazye kimekusudia kwa nia ya dhati kuanzisha ligi ya
kipekee yenye kuunganisha jamii kwa masilahi mapana ya jamii nzima ikiwemo
kufungua fulsa ya michezo kama ajira kwa vijana na kukuza vipaji kwa
kuwatangaza nje na ndani kupitia
vyombo vya habari’’ alisema Mbita.
Amesema
dira kuu ya fainali ya mapinduzi cup mwaka huu ni kuunda timu ya kata yaani
combined team na kuiwezesha kushiriki ligi kubwa za kiwilaya na mkoa pia.
Katibu
wa vijana wa Chama cha Mapinduzi, CCM wilayani humo Peter Monko, amesema vijana
wanatakiwa kushiriki kwenye michezo kwa lengo la kuwasaidia kujiajiri pamoja na
kuimarisha afya zao.
Kata
ya Mwazye inaundwa na matawi manne ya CCM, ambayo ni Kazila,nMwazye, Msoma na
Mpenje. Hivyo ligi ya mapinduzi inajumuisha timu nne ambapo kila kijiji kimetoa
timu moja kwa kingilio cha shilingi elfu thelathini (30,000/=).
Comments
Post a Comment