Chama Cha Mapinduzi CCM Wilayani Kalambo Chajidhatiti Kushinda Kwa Asilimia 99 Katika Uchaguzi Wa Serikali Za Mitaa.
Na Baraka Lusajo. Kalambo.
Chama
cha Mapinduzi CCM Wilayani Kalambo Mkoani Rukwa kimeuhakikishia umma kuwa kitashinda kwa kishindo katika uchaguzi wa serikali za mitaa kutokana na utekelezaji
sahihi wa ilani yake ya uchaguzi huku kikiwataka wananchi kujitokeza
kwa wingi katika zoezi la kujiandikisha na kupiga kura ifikapo 24 Novemba kuwachagua viongozi bora kwa
maendeleo ya Taifa.
Wilaya
ya Kalambo yenyeVitongoji 422, Vijiji 111, kata 23 na Tarafa 4 ambazo ni
Kasanga, Matai, Mwimbi na Mambwe, inakadiriwa kuwa na jumla ya watu 271,393
wakiwemo wanaume 131,285 na wanawake 140,108 ambao wote wanatakiwa kuhamasishwa
vilivyo ili washiriki uchaguzi wa Serikali za mitaa mwaka huu.
Katibu
wa Siasa na Uenezi Wilayani Kalambo
John Mbita amesema chama kimejidhatiti vilivyo kuelekea kwenye ushindi
kwani Mwenyekiti wa chama hicho kitaifa Mh. Rais Wa Jamhuri ya mungano wa
Tanzania Dr,John Pombe Magufuli
ametekeleza kwa asilimia
mia moja ahadi zote.
‘’Kila mwananchi ana haki sawa ya kugombea na kupiga kura, kama
mwana Falisafa mkongwe wa Marekani kutoka Chuo Kikuu cha Havard Profesa John
Luke kupitia nadharia yake ya uwakilishi [Represantation theory]. Hivyo
wananchi wote tujitokezeni kwa wingi
katika kujiandikisha na kupiga kura kwani
ni haki yetu ya msingi ifikapo tarehe 24 Novemba 2019 ili tupate viongozi
bora watakao tuletea maendeleo.’’Alisema mbita.
Wakiongea
kupitia maadhimisho ya uzinduzi wa ligi ya mapinduzi Cup yaliyofanyika katika kata
ya Mwazye Wilayani
humo,viongozi na makada wa chama cha mapinduzi CCM, wamesema kimsingi kila mwananchi anahaki ya kugombea na kupiga kura.
Comments
Post a Comment